Pillay ataka mauaji Myanmar yachunguzwe

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka serikali ya Myanmar kuchunguza matukio mawili kaskazini mwa jimbo la Rakhine katika kijiji kiitwacho Du Chee Yar Tan kati ya January 9 na 13 ambapo zaidi ya waislamu 40 wa Rohingya waliripotiwa kuuwawa.

Bi Pillay amesema analaani upotevu wa maisha ya watu katika eneohilona kuitaka mamlaka kufanya uchunguzi kamili na huru na kuhakikisha kwamba waathirika na familia zao wanatendewa haki. Amesema kwamba ofisi yake iko tayari kusaidia mchakato huo.

Akizungumzia taarifa za kuwekwa kizuizini kwa watu kumi huko Rohingya , kamishna huyo mkuu ameelezea wasiwasi wake kuhusu namna wanavyotendewa wakiwa kizuizini. Ameitaka serikali kuhakiisha haki za yeyote anayewekwa kizuizini na kuwaruhusu wafanyakazi wa misaada ya kiutu kufika katika kijiji husika kuwasaidia jamii husika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031