Mwakilishi wa UM Somalia aipongeza Puntland

Kusikiliza /

Nicholas Kay

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay amempongeza Rais mteule wa Puntland.

Abdiweli Mohamed Ali Gaas, aliyeteuliwa leo Jumatano na wajumbe wa wabunge wa Puntland. Grace Kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Bwana Kay amesema anampongeza spika na wabunge wote kwa juhudi zao za kuelekea mchakato wa amani wa kura ya leo. Pia amesema anathamini jukumu muhimu la viongozi wa kijadi na amewapa pongezo watu wote wa Puntland.

Bwana Kay ameongeza kuwa mbali ya kura kwenda kwa amani pia anapongeza mchakato wa kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani na uongozi bora ulioonyeshwa na Rais Abdirahman Mohamed Farole anayeoondoka.

Amesema licha ya changamoto nyingi zilizowakumba njiani , kwa kufikia muafaka na uvumilivu Puntland imefikia dhamira yake ya kumchagua kiongozi mpya wa kanda na amewatol;ea wito kuendelea kuwa na utulivu na mshikamano.

Bwana Kay amesema amehakikishiwa utekelezaji na kujizatiti kwa wadau mbalimbali kuanza mchakato wa kidemokrasia ambao ulisitishwa Julai 2013 na kuomba ushirikishwaji mkubwa wa wanawake katika mchakato wa siasa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031