Mtaalam wa Umoja wa Mataifa alaani ukatili dhidi ya waandamanaji Cambodia

Kusikiliza /

 

 

Ramana ya Cambodia

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Cambodia, Surya Subedi, ametoa wito uwepo utulivu kufuatia askari jeshi nchini humo kuwafyatulai risasi wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeza nguo waliokuwa wakiandamana, na kuwaua watu wane.

Hilo ni tukio la tatu ambalo vyombo vya dola vimefyatulia risasi umati wa watu na kusababisha vifo tangu uchaguzi wa Julai mwaka 2013 ambao matokeo yake hayakukubaliwa.

Bwana Subedi amelaani mauaji hayo na kutoa wito kwa mamlaka nchini humo kujiepusha na dhuluma dhidi ya waandamanaji.

Ametoa wito ufanyike uchunguzi huru haraka kubainisha ikiwa nguvu za kupindukia zilitumiwa dhidi ya waandamanaji, huku akielezea masikitiko yake kuwa waandamanaji wameanza kutumia ghasia na hivyo kuwaomba wadhibiti hisia zao pia.

 

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2017
T N T K J M P
« mei    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930