Mkuu wa WFP azuru Iran

Kusikiliza /

Ertharin Cousin, WFP

Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Ertharin Cousin ameanza ziara ya siku mbili nchini Iran ambako pamoja na mambo mengine pia atatembelea kambi inayohifadhi wakimbizi wa Afghanistan.

Akiwa nchini humo, Bi Cousin atakutana na kufanya mazungumzo na maafisa wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa ikiwemo wale wa Umoja wa Mataifa.

Anatazamiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari hapo siku ya Jumanne January 21.

Iran ni moja ya mshirika muhimu wa WFP kutokana na michango yake mbalimbali ya kihisani.Wakati kimbunga Haiyan kilipoipiga Ufilipino na kusababisha madhara makubwa, jamii ya wanaIranwalichangia kiasi cha dola za Marekani 100,000 kwa WFP.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031