Mkakati wa kutokomeza njaa wazinduliwa nchini Timor-Leste

Kusikiliza /

Nembo

Mkakati wa kwanza wa kutokomeza njaa katika ukanda wa Asia na Pasifiki umezinduliwa leo nchini Timor-Leste na Waziri Mkuu wa taifa hilo, Kay Rala Xanana Gusmão.

Mkakati huo ambao kwanza ulizinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon mnamo mwaka 2012, unalenga kuweka mustakhbali ambao watu wote wanafurahia haki ya kuwa na chakula, na ambapo vitega riziki na mifumo ya chakula ni thabiti ili kuweza kuhimili hali zisizotabirika, zikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati wa kuuzindua mkakati huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kijamii na Kiuchumi kwa eneo la Asia na Pasifiki, ESCAP, Noeleen Hayzer, amesema njaa ni jambo la kufeli kimaendeleo lisiloweza kusamehewa, na kikwazo kikubwa kwa kujenga mustakhbali jumuishi, endelevu na thabiti.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31