Mauaji ya kimbari CAR yananukia; lawama ni kwa jumuiya ya kimataifa: Ging

Kusikiliza /

Moja ya familia iliyosaka hifadhi kwenye mji mkuu Bangui

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu imeonya kuwa kinachoendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kinaweza kuibua mauaji ya kimbari. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

John Ging, Mkuu wa operesheni wa OCHA amefanya ziara ya siku tano huko  Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyompatia fursa ya kutembelea miji yaBangui, Bossangoa na hadi kijiji cha Zere na kujionena hali halisi ya binadamu kukata tamaa katikati ya madhila ya kutisha.

Ameonya kuwa dalili za mauaji ya kimbari ziko dhahiri na ametupia lawama jamii ya kimataifa kwa kupuuza mzozo huo unaochukua sura mpya kila uchao. Amesema miaka nenda miaka rudi mgogoro unazidi kukomaa na hoja ni kwa nini hatua hazikuchukuliwa mapema dalili zote zilipokuwa dhahiri kuelekea kinachotokea hivi sasa.

(Sauti ya Ging)

"Vitaharishi ni vya kiwango cha juu sana! Kuna dalili zote za yale tuliyoshuhudia maeneo mengine kama Rwanda, Bosnia. Viashiria vyote vipo na visababishi vipo dhahiri kwa mauji ya kimbari. Hakuna hoja kwenye hilo. Iwapo tunaweza kuchukua hatua sahihi haraka, tunaweza kubadili mwelekeo haraka zaidi kuliko vile ambavyo tunaweza kufanya kwingineko."

Bwana Ging amesema kila alipopita wananchi walikuwa wanahoji kwa nini wametelekezwa, na ametaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuwapatia majibu.

OCHA inasema kilichobakia hivi sasa ni Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye ramani ikiwa na mipaka yake lakini miundombinu ya kulifanya liwe taifa imebomoka ikiwemo taasisi za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya Laki Nane wamekimbia makaziyaona katiyaoLaki tano wanatoka mji mkuuBangui.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031