Makamu Rais Benki ya dunia kanda ya Afrika kuzuru Angola

Kusikiliza /

Makhtar Diop, Makamu Rais wa Benki ya dunia, Ukanda wa Afrika

Makamu Rais wa benki ya dunia kwa ukanda wa Afrika Makhtar Diop Jumatano anaanza ziara ya siku mbili nchiniAngola, lengo likiwa ni mazungumzo ya masuala ya maendeleo na Rais José Eduardo dosSantos, na viongozi wengine waandamizi wakiwemo mawaziri na Gavana wa Benki kuu.

Taarifa ya Benki ya dunia imesema ziara yake, ya kwanza nchini humo tangu kufanywa na kiongozi wa ngazi yake mwaka 2007, inalenga kuchagiza uhusiano naAngolana kusaidia vipaumbele vya muda mrefu vya maendeleo nchini humo.

Katika mkakati wa hivi karibuni waAngolawa mwaka 2014 hadi 2017, Benki ya dunia ilijizatiti kusaidia kipindi cha mpito cha nchi hiyo cha kuweza kukopeshwa na hivyo kufungua fursa kwa ushirikiano zaidi wa baadaye.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031