Kwa msaada wa BINUCA mamlaka ya uchaguzi CAR yaanza maandalizi

Kusikiliza /

Ramana ya CAR

Mamlaka ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati NEA imeanza kuzuru vituo mbalimbali vya uchaguzi  unaotarajiwa kumaliza uongozi wa mpito mapema mwaka 2015.

Kwa msaada wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo BINUCA mamlaka ya uchaguzi inasema hadi sasa imeshazuru vituo 11 16 kuanzia Januari 14 hadi 27. NEA ambayo ilianzishwa Desemba 2013 ni chombo huru kilicho na wajibu wa kuandaa chaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na ina wajumbe saba walioteuliwa kwa muhula wa miaka saba.

Wakati wa ziara yao wajumbe wa NEA waliambatana na wataalamu wa uchaguzi kutoka BINUCA na wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo UNDP. Rais wa NEA bwana Dieudonné Kombo Yaya, amesema nia hasa ya ziara yao ni kupata taarifa za hali ya sasa katika taasisi za majimbo, rasirimali zilizopo na nyaraka zinazohusiana na chaguzi zilizopita kama orodha ya wapiga kura, na za kuzaliwa. Ametoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu kwani hii ni hatua ya kwanza ya mchakato wa uchaguzi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930