Kutokomeza njaa ni jukumu la kila mtu: WFP

Kusikiliza /

Nembo

Kongamano la uchumi duniani limeanza leo Jumatano  huko Davos, Uswisi ambapo Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linatumia mkutano huo kuweka bayana ujumbe ya kwamba suala la kutokomeza njaa ni jukumu la kila mtu.

Mkurugenzi Mkuu wa WFP Ertharin Cousin ataungana na wabia wengine kushawishi ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma katika kubaini na kutumia fursa za kutokomeza njaa.

Taarifa ya WFP inasema ushiriki wake kwenye tukiohilohuwezesha kuibuliwa kwa mawazo na ubia kwenye kumaliza njaa duniani. WFP inasema kuwa dunia bila njaa inawezekana tu iwapo kuna juhudi za pamoja za serikali na sekta ya biashara.

Tafiti za hivi karibuni hususan ile ya gharama ya njaa barani Afrika imeonyesha kuwa utapiamlo uliokithiri kwa watoto wachanga una madhara makubwa siyo tu kwa makuzi na hata afya zao bali pia katika ushiriki wao kwenye shughuli za kiuchumi au kijamii kwenye nchi zao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031