Kundi la maigizo la IOM laanza ziara yake vijijini huko Ethiopia

Kusikiliza /

Raia wa Ethiopia waliokuwa wanaishi Saudi Arabia wakifuata taratibu ya usajili ili kurejea nyumbani

Kikundi mashuhuri cha michezo ya kuigiza kinachoratibiwa na Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kimeanza ziara yake vijijini nchiniEthiopiaikilenga zaidi maeneo yenye wahamiaji wasio halali huko Amhara, Tigray na Oromia.

Idadi ya raia waEthiopiawanaorejea nyumbani kutokaSaudi Arabiaambako walikuwa wanaishi bila vibali imeongezeka na kufikia 154,000 na hivyo maigizo hayo yanalenga kuelimisha madhila ya kuishi ugenini bila kibali.

Maigizo hayo yanatumia muziki na baada ya kila onyesho wahusika wanaelimisha umma juu ya madhila hayo ikiwemo manyanyaso, vipigo, kuondolewa viungo vya ndani vya mwili na hata kuuawa.

KikiwaEthiopia, kikundi hicho kiitwacho Mutach kitafanya maonyesho yake pia kwenye shule, na kinatarajiwa kufikia watu Elfu Sitini hadi kitakapohitimisha ziara hiyo tarehe 28 mwezi huu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930