Kundi la kuchukua hatua lataka ghasia zikomeshwe mara moja nchini Syria

Kusikiliza /

Mkimbizi wa Syria na wanawe katika kambi ilioko Lebanon. Wanakabiliwa na mahitaji kama mamilioni ya wengine

Wanachama wa kundi la kuchukua hatua kuhusu hali nchini Syria, wamekutana leo kufuatia hali inayosikitisha nchini Syria na kulaani vikali mauaji yanayozidi kuongezeka nchini humo, uharibifu na ukiukwaji wa haki za binadamu ulokithiri.

Mkutano huo wa Kundi la kuchukua hatua ulijumuisha uanachama wa Uchina, Ufaransa, Urusi, Uingereza, Uturuki, Iraq, Kuwait, Qatar, pamoja na Umoja wa Mataifa, Muungano wa Nchi za Kiarabu na Muungano wa Ulaya, na kusimamiwa na Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Nchi za Kiarabu, Lakhdar Brahimi.

Katika taarifa ya pamoja, wameelezea kusikitishwa na kushindwa kuwalinda raia, kuongezeka kwa ghasia, uwezekano wa kuwepo machafuko zaidi nchini na mwelekeo wa kikanda wa tatizo la Syria.

Wamesema mwelekeo na ukubwa wa mzozo huo unahitaji msimamo wa pamoja na hatua za kimataifa.

Wametaka ghasia zikomeshwe mara moja, na pia kutoa mwongozo wa kuanza kutekeleza hatua za vipengee sita vilivyotokana na mkutano wa Geneva wa mwezi Juni mwaka 2012.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031