Kilimo uti wa mgongo wa ukuaji uchumi Afrika: FAO

Kusikiliza /

Wakulima shambani nchini Burundi

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema Kilimo kinapaswa kusalia kuwa injini ya ukuaji wa uchumi barani Afrika na hivyo barahilolinapaswa kukitumia ili kutokomeza njaa na kuinua uzalishaji endelevu wa chakula. Taarifa zaidi na George Njogopa.

 (Taarifa ya George)

Akizungumza hukoAddis Ababa, Bwana da Silva ameongeza wito kwa kusema kuwa Afrika inapaswa kuongeza juhudi.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kila mtu mmoja kati ya watano walioko barani Afrika wamekumbwa na kile alichokiita " kunyimwa haki ya chakula"

Huku akitaja mafanikio yanayoendelea kujitokeza ya ukuaji uchumi barani Afrika, da Silva amesisitiza kuwa barahilolinanguvu ya kubadili sura ya mambo.

Amesema kuwa mabadiliko hayo ni pamoja na kuhakikisha kwamba kasi ya ukuaji uchumi inaowanishwa na shughuli za kilimo, kuendeleza maeneo ya vijijini na kuwapiga jeki kwa hali namalimakundi ya wanawake na vijana.

Takwimu zilizopo sasa kuhusu idadi ya watu barani Afrika zinaonyesha kuwa, kiasi cha asilimia 75 ya watu wake ni wale wenye umri wa miaka 25 ama chini ya umri huo ambao wanaendelea kuishi maeneo ya vijijini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031