Kemikali za sumu kutoka Syria kuhamishiwa kwenye meli ya kimarekani huko Italia.

Kusikiliza /

Meli ya kimarekani, Cape Ray ambako kemikali zitahamishiwa. (Picha-OPCW)

Serikali ya Italia imekubali bandari yake ya Gioia Tuaro iliyoko bahari ya Mediterranean kutumika wakati wa zoezi la kuhamisha kemikali za sumu kali zaidi kutoka kwenye meli za mizigo na kuzipakia kwenye meli ya kimarekani, MV Cape Ray.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la kupinga kemikali za sumu, OPCW, Balozi Ahmet Üzümcü,  amethibitisha hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Roma, Italia baada ya kuhutubia bunge la nchi hiyo kuhusu mpango wa usafirishaji wa kemikali hizo za sumu kutokaSyriakwa njia ya bahari.

Balozi Üzümcü amesema ili kuhakikisha kemikali hizo hazileti madhara, meli hiyo ya kimarekani imefungwa mitambo miwili ya kupunguza makali ya sumu wakati chombo hicho kikiwa baharini. Amesema kuhakimishia shehena hiyo wakati chombo kimetia nanga bandarini kutaongeza usalama na kuhakikisha ulinzi wa operesheni hiyo.

Ametoa hakikisho kuwa wanaweza kutimiza ukomo wa kukamilisha kazi ya kutokomeza mpango wa silaha za kemikali nchin iSyria ifikapo katikati ya mwaka huu, huku akishukuru Italia kwa vile inavyojitoa kusaidia mchakato huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2015
T N T K J M P
« ago    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930