Kampeni maalum ya UM ya kuwafikia wasiofikika Syria yaonyesha mafanikio

Kusikiliza /

 

Mitandao

Kampeni ya siku tatu ya Umoja wa Mataifa isiyokuwa ya kawaida iliyohusisha mitandao ya kijamii ikiwamo twiter na face book imewafikia zaidi ya watu milioni 31 na wengine mamilioni wakipaza sauti zao kutaka pande zinazohusika na mgogoro nchini Syria kuruhusu  misaada iwafikie watu walioko Yarmouk eneo lililoko karibu naDamascusambako wakimbizi wa Palestina walioko Syria wamehifadhiwa.

Mashiruika ya UMkamala kuhudumia watoto UNICEF, la wakimbizi UNHCR la chakula WFP la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na lile la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA pamoja na mashirika mengina ya kimataifa ya haki za binadamu yalikuwa kinara katika kampeni hii. Msemaji wa UNRWA Chris Gunness amesema mamailioni ya watu wamesikia ombi lao hasa kwa kuzingatia taarifa za njaa kwa watoto, watoto kuugua matege na wanawake kufa kutokana na kujifungua kutokana na kukosa huduma za kitabibu.

Kampeni hii ilipigiwa chapuo na watu mashuhuri akiwamo mwigizaji Mia Farrow kutoka Marekani ambaye ni balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Unicef, mwanamuziki nguli, Muahmed Assaf kuitoka uarabuni, mwigizaji kutoka Uingereza Hugh Grant

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29