IOM yapanua wigo wa msaada Sudan Kusini na yatoa ombi la kimataifa

Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa IOM akizungumza na Mkuu wa IOM Sudan Kusini katika kituo cha UNMISS, JUBA

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linapanua wigo wa msaada wake kwa watu waliotawanywa na machafuko yanayoendelea Sudani Kusini  na limetoa ombi kwa jumuiya ya kimataifa kupata msaada zaidi.

Mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing amewasili Juba Jumapili ili kuonyesha hofu yake na mshikamano kwa watu walioathirika na machafuko , na pia kukutana na wafanyakazi wa IOM na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu. Malazi,chakula, huduma za afya, maji na usafi ni vinahitajika haraka katika maeneo yanayohifadhi wakimbizi wa ndani. Christiane Berthiume ni msemaji wa IOM

(SAUTI YA CHRISTIANE BERTHIUME)

Kwa sasa IOM inaendelea na uandikishaji wa wakimbizi wa ndani mjini Juba na kuwapatia vifaa muhimu vya misaada kama vile mablanketi, vifaa vya malazi na vile vya kupikia ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha maisha yao na kuishi maisha ya kawaida kwani wengi walikimbia na kuacha vitu vyao kabisa."

Vita vilizuka Sudan Kusini Desemba 15 na tangu wakati huo vimewalazimu kugungasha virago watu takribani 200,000. Inakadiriwa kuwa watu 62,000 wamepata hifadhi na ulinzi kwenye ofisi za Umoja wa mataifa na wengine 22,600 wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930