IOM kuanza kuwasafirisha wahamiaji walioko CAR.

Kusikiliza /

Wananchi waliosaka hifadhi kwenye uwanja wa ndege kwenye mji mkuu Bangui, CAR (Picha-IOM)

Shirika la uhamiaji duniani IOM, kesho linatarajia kuanza kuwasafirisha kwa ndege maelfu ya wahamiaji wa nchi mbalimbali walioko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambao wametatizika kufuatia mgogoro unaoendelea nchini humo.

Zaidi ya wahamiaji Elfu 60 kutoka nchi jirani wameshapelekea maombi kwenye balozi zao CAR. IOM imepokea maombi ya kuwaondoa wahamiaji kutoka Chad , Mali, sudan na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC . Takribani wahamaiji 27, 000 wameshahamishwa na serikali zao huku wengine 33, 000 wakihitaji msaada wa dharura ili kuondoka nchini humo. IOM inahitaji dola milioni 17.5 kuwahamisha wahamiaji elfu kumi kutoka CAR na kusaidia wahamiaji 50,000 kujenga upya maisha yao baadaya ya kurejea nyumbani. Chris Lom ni msemaji wa IOM

(Sauti ya Lom)

"Fedha hizi zitaelekezwa kusaidia gharama za wanaorejea kwenye vituo wanavyooingilia, usafiri wa ndani, vifaa vya usaidizi wanapofika na kusaidia kutangamana katika mazingira mapya kwani wengi wao wanarejea kwenye nchi maskini sana."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2014
T N T K J M P
« nov    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031