Ingawa mafanikio yaliyopatikana mazungumzo ya Syria ni kidogo kuna matumaini:Brahimi

Kusikiliza /

Lakhdar Brahimi

Pande mbili zinazokinzana nchini Syria zimekamilisha duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani mjini Geneva Ijumaa , huku kukiwa na hatua ndogo sana iliyopigwa, amesema Lakhdar Brahimi, mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Muungano wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria.

Amesema ingawa pande zote zimeshiriki mazungumzo hayo katika njia inayokubalika lakini pengo baina ya pande hizo mbili ni kubwa.

Ameongeza kuwa kutokuwa na hatua kubwa kwenye mazungumzo hayo kumeongeza simanzi kwa mamilioni ya Wasyria. Hata hivyo amesema pande zote zimejidhatiti kutekeleza tamko la kupata suluhu ya kisiasa.

(SAUTI YA LAKHDAR BRAHIMI)

" Wakati wa majadiliano yetu niliona kidogo mtazamo wa pamoja pengine zaidi hata ya pande hizo mbili zilivyoona.Pande zote zinajua kwamba kutekeleza tamko la Geneva ni lazima wafikie muafaka wa kumaliza vita na kuanzisha serikali ya mpito yenye mamlaka yote. Kiongozi miongoni mwao, majadiliano ya kitaifa, kutathimini katiba na kufanya uchaguzi.Pande zote zinaelewa kwamba vita nchini mwao vimesababisha madhila yasiyokubalika kwa watu wa Syria. Wote wanatambua haja ya kumaliza machafuko haraka.Tunatumai pia wataongeza mara mbili juhudi za kupata fursa haraka ya kupunguza kiwango cha machafuko nchini humo. Kwa Wasyria wote walionasa katika vita kazi yetu itaonekana inaenda polepole mno, naelewa hilo.Lakini tunajaribu kukabiliana na suala gumu saana ambalo limesababisha vita hivi, na kwa bahati mbaya ni suala linalochukua muda"

Wajumbe wa pande zote wanatarajiwa kurejea tena Geneva Februari 10 kuanza duru nyingine ya majadiliano.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031