ICRC yaziunganisha familia kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maandishi huko Sudan Kusini

Kusikiliza /

Wakimbizi wa Sudan Kusini kufuatia mapigano nchini humo

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu (ICRC) imefanikiwa kuwaunganisha watu zaidi ya 650  na familia zao. Familia hizo zilitenganishwa wakati zikikimbia mapigano ya karibuni nchini Sudan Kusini.

ICRC inabaini ndugu wa familia hizo katika maeneo waliyokimbilia kutafuta usalama na inawaunganisha na jamaa zao kwa njia ya simu na ujumbe mfupi wa maandishi wa simu za mkononi . Jacob Custer ni msemaji wa ICRC mjini Juba

(SAUTI YA JACOB CUSTER)

"Kupitia njia hizi tumeweza kujaribu kusaidia watu kuwasiliana na  familia zao ambao wamepotezana, ili waweze kufahamu hali zao na iwapo wako salama. Kwa kufahamu familia zao ziko salama kunatia moyo sana kwani tunashuhudai watu wakitabasamu na kufurahi na wanashukuru sana kwa kuweza kuwasiliana na familia zao."

Njia kama hiyo ya kuziunganisha familia pia inatumiwa na Umoja wa mataifa na shirika la Save the children.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930