Hofu ya usalama yatishia wananchi kurejea Bangui: IOM

Kusikiliza /

Watu wa CAR Warudishwa nyumbani wanopewa kipaumbele ni wanawake na walio na mahitaji ya kiafya

Idadi kubwa ya watu waliosaka hifadhi kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui na viunga vyake wamelieleza shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kuwa hofu ya usalama ni sababu kuu ya wao kugoma kurejea makwao.

Katika utafiti huo wa kwanza ulioendeshwa na IOM kwa ushirikiano na wadau wake kwenye maeneo 46 mjini Bangui, watu 587 walihojiwa iwapo wanapenda kurejea makwao na sababu za kuchelewa kurejea.

Asilimia 99 walitaja hofu ya usalama kuwa ni kikwazo huku asilimia 85 wakisema watarejea tu iwapo kwenye makazi yao kutakuwepo na vikosi vya ulinzi ili kuhakikisha usalama wao.

Kuhusu sababu za kusaka hifadhi Bangui, theluthi moja walisema kuwa kuchomwa moto kwa nyumba zao na hata kuporwa mali zao kulichochea wao kukimbia, huku asilimia 92 wakisema kuwa walilazimika kuacha kazi kutokana na kupoteza makazi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930