Fao yawasaidia wakulima wa Ufilipino kujikwamua baada ya Kimbunga Haiyan

Kusikiliza /

Kimbunga Haiyan kilikwamisha juhudi za kilimo

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, limeanza kuwapa afueni wakulima wapatao 44,000 nchini Ufilipino, ambao waliathiriwa na kimbunga Haiyan, kwa kuwapa mbegu zenye ubora wa hali ya juu ili kuwasaidia kujikwamua tena baada ya uharibifu wa kimbunga hicho mnamo Novemba 8, 2013.

Taifa la Ufilipino lilipoathiriwa na kimbunga Haiyan, wakulima walikuwa wanajiandaa kwa mavuno ya mpunga, huku wakitarajia mazao mazuri. Kimbunga hicho kiliathiri vibaya mno mazao hayo, pamoja na maghala ya mbegu za kupanda kwa msimu mpya.

Shirika la FAO limefanya kuwawezesha wakulima kupanda tena kwa msimu wa kupanda wa Disemba na Januari jambo la kipaumbele, ili kuhakikisha kuwa wakulima hao wanakwamua tena vitega riziki vyao. Kufikia sasa, Shirika la FAO likishirikiana na Idara ya Kilimo, limegawa zaidi ya asilimia 54% ya mbegu zinazohitajika kwa wakulima walioathiriwa na Kimbunga Haiyan.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031