FAO imeaanza kugawa mbegu kwa wakulima walioathirika na kimbunga Haiyan Ufilipino

Kusikiliza /

Waziri wa maswala ya kigeni wa Norway Børge Brende, akiwa na wakulima Ufilipino

Miezi miwili baada ya kimbunga Haiyan kukumba Ufilipino waziri wa mambo ya nje wa Norway Børge Brende, amelipongeza shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO kwa kazi yake ya kuwasaidia wakulima wa mpunga kwa mbegu ili kuziba pengo la mazo waliyopoteza kwenye kimbunga.

Brende amewatembelea wakulima wa kijiji cha Tingib jimbo la Samar Mashariki mwa mkoa wa Visayas eneo ambalo liliathirika saana na kimbunga Haiyan hapo tarehe 8 Novemba mwaka jana na kuikatili maisha ya watu zaidi ya 600, kusambaratisha sekta ya kilimo na pia ya uvuvi.

Waziri Brende amesema mbegu ni ishara ya ahueni na anajua ni jinsi gani muhimu kwa wakulima kupanda upya mazao wakati huu kabla hawajachelewa.

Brende amezungumza na wakulima na binafsi kuwapa mifuko ya mbegu, kuzuru mashamba ya mpunga ambako serikali ya Norway iligawa mbegu na kuishukuru FAO kwa kazi iliyofanya hadi sasa.

FAO kwa msaada wa serikali ya Norway na ushirikiano na serikali ya Ufilipino wameweza kupata mifuko ya mbegu kwa ajili ya msimu wa kupanda wa Desemba na Januari.Mgao mwingine wa mbegu ulifanyika wiki tatu zilizopita.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031