Bei ya chakula duniani ingali ya juu japo haijayumba:FAO

Kusikiliza /

Soko la Chakula

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema bei ya chakula duniani bado ni ya juu na mwaka 2013 ni miongoni ya miaka iliyoweka rekodi ya gharama ya juu ya chakula. Flora Nducha na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Kwa mujibu wa orodha ya gharama za chakula ya FAO mwezi Desemba mwaka 2013 wastani ulikuwa pointi 206.7 ukiwa hauna mabadiliko makunbwa na mwezi Novemba, huku kukiwa na ongezeko la bei kwa bidhaa za maziwa na nyama, wakati vitu kama sukari, nafaka na mafuta zikipungua.

FAO inasema ingawa wastani wa point mwaka 2013 ni 209.9 zikiwa chini kidogo ya 2012 na 2011 lakini bado inashika nafasi ya tatu kwa miaka iliyokuwa na gharama za juu sana za bidhaa. Abdolereza Abbassian ni mchumi katika shirika la FAO.

(Sauti ya Abdolereza)

Mchumi huyo amesema mwelekeo unaonyesha matumaini kwa bei za vyakula mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka jana.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031