Baraza la Usalama lataka masuala muhimu ya mzozo wa Mali yashughulikiwe

Kusikiliza /

Wanachama wa Baraza la Usalama wamekaribisha kufanyika kwa uchaguzi wa urais na ubunge hivi karibuni nchini Mali, kama hatua muhimu ya kurejesha uongozi wa kikatiba nchini humo.

Wanachama hao ambao wamesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu ilowasilishwa na Mwakilishi wake nchini Mali, Albert Koenders, wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza harakati jumuishi za kisiasa, ambazo zitaleta maridhiano na kukabiliana na masuala muhimu yanayozozaniwa, bila mashartti. Baadaye, rais wa Baraza hilo, ambaye ni mwakilishi wa Jordan, amesoma taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kilichojadiliwa.

"Wameelezea masikitiko yao kuhusu matukio ya ghasia na ugaidi hivi karibuni kaskazini mwa nchi hiyo, na kuhusu na kuelezea umuhimu wa kupinga vitendo kama hivyo na kutoa uungaji mkono unaofaa wa kiusalama, kiuchumi na kijamii, ili kuzuia kuibuka tena kwa makundi ya kigaidi na vitendo vyao."

Wamesisitiza pia umuhimu wa kuviwezesha vikosi vya ujumbe wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA, kuetekeleza majukumu yake kikamilifu katika nafasi zake zote, zikiwemo polisi, wanajeshi na wahudumu wa kiraia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031