Baraza la haki za binadamu kufanya kikao maalumu kuhusu CAR

Kusikiliza /

 

Baraza la haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu litafanya kikao maalumu Jumatatu tarehe 20 Januari kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ombi la kufanyika kikao hicho limewasilishwa leo kwa njia ya barua na mwakilishi wa Ethiopia kwenye baraza hilo kwa niaba ya kundi la Afrika. Barua hiyo imetiwa saini nchi wanachama 36 wa baraza la usalama na wajumbe 43 waangalizi.

Miongoni mwa nchi wanachama waliotia saini na kuunga mkono ni pamoja na mataifa  manne ya Afrika Mashariki ambayo ni Tanzania, Kenya, Rwanda na Burundi na majirani wa CAR ambao ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Chad, Sudan Kusini na wahusika Jamhuri ya Afrika ya Kati.Ilikikao hicho maalumu kifanyike kinahitaji uungwaji mkono wa wanachama 16 au zaidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2016
T N T K J M P
« jul    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031