Ban ziarani Cuba, asema amani,usalama na maendeleo kumulikwa

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipowasili Cuba akiwa na waziri wa biashara za kigeni Rodrigo Malmierca

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko ziarani nchini Cuba kuhudhuria mkutano wa jamii ya Amerika Kusini na mataifa ya Caribbean, CELAC.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili nchini humo Bwana Ban amezungumzia matarajio yake katika ziara hiyo ambayo pia inajumuisha kumbukumbu shujaa wa Cuba na Latin Amerika José Marti.

(SAUTI YA BAN)

“Natarajia kusikiliza maoni kuhusu masuala ya msingi ikiwamo usalama na amani pia maendeleo andelevu na haki za binadamu. Natarajia pia kukutana na maafisa wa Cuba akiwemo rais Raul Castro na mawaziri wengi. Tutajadili masuala mengi kuhusu maendeleo amani, usalama na mafanikio. Cuba inapitia kipindi muhimu cha mchakato wa mabadiliko nina shauku ya kujifunza na kuzungumza namna Umoja wa Mataifa unavyoweza kuendelea kusaidia katika mchakato huu.”

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031