Ban azungumzia maendeleo ya kuteketeza silaha za kemikali Syria

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesifu maendeleo yaliyopatikana katika utokomezaji wa mpango wa silaha za kemikali nchini Syria, hususan habari za hivi karibuni kuhusu kusafirishwa kwa shehena ya kwanza ya vifaa muhimu vinavyohusiana na mpango huo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema Bwana Ban amepokea rasmi taarifa ya kung'oa nanga kwa meli ya vifaa hivyo kutoka bandari ya Lattakia nchini Syria tayari kwa kufanyiwa uthibitishwaji na kuteketezwa nje ya nchi hiyo kwa mujibu wa azimio la baraza la usalama.

Katibu Mkuu amesema hatua hiyo ni ya kuungwa mkono na kwa mara nyingine tena amempogeza Mratibu wa jopo la pamoja la Umoja wa Mataifa na OPCW linalosimamia kazi hiyo, Bi. Sigrid Kaag pamoja na timu yake kwa kutekeleza jukumu lao kwa kasi licha ya mazingira magumu yanayowakabili.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930