Ban atoa wito kwa wanaopigana kusitisha mapigano kwa ajili ya Olimpiki

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa pande zote zilizopo kwenye migogoro ya silaha kuweka silaha chini na kusitisha mapigano kwa ajili ya mbiu ya amani ya Olimpiki, kabla kuanza michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi mjini Sochi, Urusi.

Bwana Ban amesema washiriki katika michezo hiyo watabeba bendera za nchi tofauti, lakini wanakuja pamoja chini ya bendera moja ya usawa, kucheza kwa haki, kuheshimiana na kutobaguana. Ametoa wito kwa wote wanahusika katika michezo hiyo, zikiwemo serikali, makundi, mashirika na watu binafsi, kutunza na kulinda maadili hayo muhimu ya Olimpiki.

Ban amesema anapotoa mbiu ya amani mwaka huu, anawawazia watu wa Syria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na wote wanaoteseka kutokana na machafuko yasiyo na maana, zikiwemo familia zilizowapoteza wapendwa wao katika shambulizi la bomu hivi karibuni, huko Volgograd, ambayo si mbali sana na Sochi.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031