Ban atangaza tume ya kuchunguza matukio CAR tangu Januari 1 2013

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametangaza tume ya uchunguzi katika matukio nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu Januari 1 mwaka 2013, kufuatia ombi lililotolewa na Baraza la Usalama kwamba tume hiyo iundwe, katika azimio lake 2127(2013) la Disemba 5, 2013.

Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa Jumatano jioni na msemaji wa Katubu Mkuu, tume hiyo itajumuisha wataalam katika masuala ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu. Wataalam hao ni ni Jorge Castañeda wa Mexico, Fatimata M'Baye wa Mauritania na Bernard Acho Muna wa Cameroon, ambaye atakuwa mwenyekiti wa tume hiyo.

Jukumu la wataalam hao litakuwa ni kuchunguza ripoti za ukiukwaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa ujumla katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao umetekelezwa na pande zote katika mzozo tangu tangu Januari mosi mwaka 2013. Watahitajika kuandaa maelezo, kusaidia kuwatambua walotekeleza ukiukwaji na uhalifu huo na kusaidia kuhakikisha kuwa wanaowajibika na vitendo hivyo wanafikishwa mbele ya sheria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031