Ban ataka amani Misri ikipiga kura ya maoni

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anafuatilia kwa karibu mchakato wa kura ya maoni nchini Misri.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Katibu mkuu mjini New York imemkariri Bwana Ban akisema anasisitiza umuhimu wa kuheshimu uhuru wa kukusanyika na kujieleza pamoja na ahadi ya kutofanya vurugu.

Katibu mkuu amewhamasisha raia wote wa Misri kuhakikisha awamu ijayo ya mpito inafanyika katika njia jumuishi, ya amani na uwazi.

Kadhalika Bwana Ban ametaka raia wan chi hiyo kuelezea tofauti zao bila ghasia huku pia akirejelea uungwaji mkono kwa nchi hiyo kutoka Umoja wa Mataifa katika utawala wa mpito ambao unafuata misingi ya kanuni za kidemokrasia na haki za binadamu kwa wananchi wote wa Msri.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31