Ban asikitishwa na shambulio la bomu Lebanon

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari kusini mwa mji wa Beirut katika mtaa wa makazi na biashara uitwao Haret Hreik na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa.

Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kwa waathirika wa tukio hilo na kwa serikali na watu wa Lebanon na kutaka watekelezaji wa shambulio hilo wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Amesema vitendo mfululizo vya mashambulizi ya kigaidi nchini Lebanon havikubaliki na katibu mkuu na kutaka pande zote nchini humo kuja pamoja ili kusaidia katiba ya nchi hususani vikundi vya kijeshi na kuhakiisha umoja wa kitaifa kama njia muhimu ya uslama wa Lebanon dhidi ya ugaidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031