Ban akaribisha kuchaguliwa kwa rais wa mpito Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza /

Bi. Catherine Samba-Panza, Rais mpya wa mpito nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha kuchaguliwa kwa Bi Catherine Samba Panza kuwa rais mpya wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa njia ya uwazi ilosimamiwa na baraza la kitaifa la mpito.

Katika taarifa ilotolewa na msamaji wake, Bwana Ban amempa hongera Bi Samba Panza kwa uchaguzi huo, na kuwapongeza wote waloshiriki katika uchaguzi huo, huku akitazamia uteuzi wa Waziri Mkuu kwa siku chache zijazo kwa matarajio makubwa.

Amesema kubadili kwa uongozi nchini humo kunatoa fursa muhimu ya kurejesha harakati za mpito kwenye mkondo unaotakiwa.

Ban pia bado anasikitishwa na ghasia za kidini zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, na hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930