Ban aitaka serikali ya Sudan Kusini kuheshimu sheria ya kimataifa na kuwalinda raia

Kusikiliza /

Waathiriwa wa ghasia Sudan Kusini wanaokimbilia ofisi ya UNMISS kutafuta hifadhi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ameelezea kushangazwa na kusikitishwa na jaribio la maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Sudan Kusini kuingia kwa nguvu kwenye eneo la kutoa ulinzi kwa raia katika ua la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS mjini Bor.

Bwana Ban amesema maelfu ya raia wameuawa, wengine kukiukwa haki zao na kuachwa bila makazo katika mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja nchini humo, na kutoa wito kwa viongozi wa pande zinazozozana kufanya juhudi zaidi kuhakikisha kuwa wapiganaji walioko chini ya amri yao wanawalinda raia na kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Amewataka pia wasitishe mapigano hayo, ambayo yamekuwa na madhara makubwa kwa taifa lao changa.

Ban ametiwa wasiwasi kwa kusikia kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walitishwa na wanajeshi wa Sudan Kusini pale walipokataa kuwaruhusu wanajeshi wenye silaha kuandamana na raia wanaotembelea eneo la kuwapa hifadhi salama wakimbizi. Amesema tukio hilo ni moja tu ya matukio mengi ya kukiuka mkataba kuhusu vita, na hivyo kufanya vigumu UNMISS kutekeleza na majukumu yake na kuwaweka wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa hatarini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930