Bado kuna tofauti kubwa za kijamii licha ya hatua za maendeleo: UNDP

Kusikiliza /

Ripoti mpya ya Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP, imesema upunguzaji endelevu wa pengo lililopo la usawa unahitaji kubadili mwenendo na kuzingatia ukuaji jumuishi zaidi, ambao unaungwa mkono na sera zinazochagiza kumiminika zaidi kwa rasilmali kwa wote, na mienendo ya kijamii.  

Ripoti hiyo ambayo imezinduliwa leo na Mkuu wa UNDP, Helen Clark, imesema kuwa asilimia 1 ya walio tajiri zaidi duniani wanamiliki asilimia 40 ya utajiri wote duniani, huku nusu ilosalia kwenye daraja ya chini ikiwa haina hata asilimia 1 ya utajiri wote.

Ripoti hiyo iitwayo, "Ubinadamu ulogawika: kukabiliana na mwanya wa kijamii katika nchi zinazoendelea," inaonyesha kuwa ikiwa hali hii haiatashughulikiwa, ukosefu wa usawa unaweza kudhoofisha misingi ya maendeleo na amani ya kijamii na kitaifa.

Bi Clerk, Mkuu wa UNDP, amesema ukosefu wa usawa uliopo kwa viwango vya sasa kunaonyesha kutokuwepo haki, na pia kuwa kizuizi cha maendeleo ya mwanadamu.

Tipoti hiyo inamulika vianzo na madhara ya mianya inayowagawa wanadamu kati ya tajiri na maskini ndani ya nchi na baina ya nchi mbalimbali, na kusema kuwa hakuna msingi wowote wa kukubalika kuhusu ukuaji wa mwanya kati ya matajiri na maskini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930