Nyumbani » 28/01/2014 Entries posted on “Januari 28th, 2014”

Ban akutana na Fidel Castro: Wajadili Syria, Sudan Kusini na mengineyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye yuko ziarani nchini Cubaamekuwa na mazungumzo na Rais wa zamani wa nchi hiyo Fidel Castro Ruz mjini Havana. Msemaji wa Katibu amesema katika taarifa kuwa wawili hao wamekuwa na mazungumzo kuhusu masuala ya kimataifa ikiwemo Syria, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na ile ya [...]

28/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban aisifu Cuba kwa mchango wake kwenye tiba, asema ni wa kuigwa

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa shule huko Havana, Cuba wakati wa ziara yake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea chuo kikubwa zaidi ya tiba duniani kilichoko nchini Cuba kijulikanacho kama ELAM na kushukuru nchi hiyo kwa vile ilivyo mstari wa mbele kwenye kuimarisha ushirikiano wa nchi za Kusini hasa kwenye masuala ya tiba. Akizungumza kwenye chuo hicho amesema mchango huo wa kihistoria wa Cuba uko dhahiri kwani [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya Geneva yasuasua lakini kuendelea Jumatano

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi,Mwakilishi Maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Nchi za Kiarabu

Mwakilishi Maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Nchi za Kiarabu, Lakhdar Brahimi, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa amezishauri pande zinazohusika katika mazungumzo ya amani kuhusu Syria kuahirisha kikao cha Jumanne mchana, ili zipate fursa ya kujiandaa tena na kurejelea kikao bora zaidi cha mazungumzo hayo hapo kesho Jumatano asubuhi. [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma kwa wagonjwa walio taabani ni zaidi ya tiba: Ripoti mpya

Kusikiliza / Ripoti

Mtu mmoja kati ya watu 10 ndiye anayepata huduma ya tiba ya kupunguza maumivu ya magonjwa anapokuwa taabani na kukaribia kupoteza maisha, imesema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumanne ikitaka mataifa kujumuisha huduma hiyo ya tiba kwenye mifumo yao ya afya. Ripoti hiyo ikionyesha mahitaji ya huduma hiyo duniani kote imechapishwa kwa ushirikiano [...]

28/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Raia wa Somalia waishio Ughaibuni waanza kurejea nyumbani!

Kusikiliza / Mradi wa matofali Somalia

Wakati ujenzi wa taifa la Somalia ukishika kasi , raia wazawa nchini humo wameamua kurejea nyumbani wakati huu ambapo usalama unatajwa kuimarika katika taifa hilo ambalo limetatizika kwa machafuko kwa muda mrefu sasa. Nini kinachowafanya raia hao waliokuw aughaibuni kurejea makwao? Ungana an Joseph Msami katika ripoti inayofafanua zaidi

28/01/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wananchi Sudan Kusini wamekata tamaa wanataka wahamishwe: Mkuu OCHA

Kusikiliza / Bi. Amos akiwa kwenye moja ya kambi za muda huko Sudan Kusini

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya usaidizi wa kibinadamu Bi. Valerie Amos ametembelea Malakal ambao ni mji mkuu wa jimbo laUpper Nilenchini Sudan Kusini na kushuhudia hali ya taabani inayokumba maelfu ya raia walio kwenye makazi ya muda ndani ya ofisi ya ujumbe wa Umoja huo, UNMISS. Bi. Amos ambaye [...]

28/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali CAR na Burundi

Kusikiliza / Baraza la Usalama

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekutana leo kujadili hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na pia kujadili hali nchini Burudi, likizingatia ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu ofisi ya Umoja wa Mataifa Burundi. Joshua Mmali na taarifa kamili (Taarifa ya Joshua) Baraza la Usalama limeanza shughuli zake hii leo kwa kupitisha kwa [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunisia yapongezwa kwa kuanzisha katiba mpya, yapewa angalizo.

Kusikiliza / Ravina Shamdasani

Msemaji wa Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani ameipongeza Tunisia kwa hatua ya kupitisha katiba mapya siku ya jumapili ambayo amesema inatafsiri matarajio ya utu, haki ya kijamii na ukombozi wa mtu binafsi. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bi Shamdasani pia amepongeza mfano wa kujitoa katika mazungumzo [...]

28/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Licha ya mafanikio, Rwanda iweke fursa ya demokrasia ya kweli: Mtaalamu UM

Kusikiliza / Maina Kiai

Mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kufanya mikutano ya amani na haki ya kujumuika, Maina Kiai, amesifu Rwanda kwa maendeleo yake ya kiuchumi miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari huku akitaka nchi hiyo kuondoa vikwazo dhidi ya mijumuiko ya amani. Amesema hatua hiyo itawezesha kupanua wigo wa mafanikio yake hadi kwenye [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake ni ukiukwaji mkubwa zaidi wa haki duniani: Ban

Kusikiliza / Ukatili dhidi ya wananaweke

Ujumbe wetu uko bayana, wanawake na watoto wana haki ya kujisikia salama na kuishi maisha yenye utu mahali popote pale iwe kwenye mapigano, amani, umaskini au ustawi! Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon katika kampeni ya UNiTE, iliyofanyika Havana Cuba, ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake. Bwana Ban amesema [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa WFP wa mchele na unga wa mahindi wawasili Bangui CAR

Kusikiliza / Mgao wa mahindi CAR

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema Jumatatu malori yake yaliyosheheni msaada wa tani 250 za mchele na unga wa mahidi yamewasili mjini Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.  Malori hayo yamewasili baada ya safari ya kilometa 600 kutoka mpakani mwa Cameroon. Malori hayo ni sehemu ya msafara wa [...]

28/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka wakimbizi wa Somalia wasilazimishwe kurejea makwao

Kusikiliza / Wanawake wakimbizi wa Somalia wakisubiri mgao wa kuni kaskazini mashariki mwa Kenya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa upya ombi la kutaka mataifa yanayohifadhi wakimbizi waSomaliakutowalazimisha kurejea makwao hususan maeneo ya kati nay ale ya kusini. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace Kaneiya) UNHCR imesema ijapokuwa usalama umeikarika kwenye maeneo hayo ya kusini na kati ikiwemo mji mkuu waSomalia, Mogadishi, bado [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji zaidi ya 45,000 walihatarisha maisha yao 2013 kuingia Italia na Malta:IOM

Kusikiliza / Watu wanaoelekea Italia kwa kutumia boti

Wakimbizi zaidi ya 45,000 walihatarisha maisha yao mwaka 2013 wakijaribu kuvuka bahari ya Mediteraniani ili kuingia Italia naMalta limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Idadi ya wahamiaji waliowasili ni kubwa zaidi tangu mwaka 2008, ukiacha mwaka 2011 ulioghubikwa na mgogoro waLibya. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji zaidi ya 42,900 waliwasili Italia na wengine 2,800 [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada ya kibinadamu bado haijafika Homs:UM

Kusikiliza / WFP, Syria

Mashirika ya misaada ya Umoja wa mataifa nchini Syria bado hayajapata ulinzi unaotakiwa ili kuwawezesha kufikisha misaada ya kibinadamu inayohitajika haraka kwa maelfu ya raia waliokwama kwenye mji wa Homs. Flora Nducha na maelezo kamili (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema liko tayari kupeleka mgao wa chakula kwa familia [...]

28/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930