Nyumbani » 24/01/2014 Entries posted on “Januari 24th, 2014”

IOM imepeleka msaada wa majira ya baridi kwa Wasyria walioko Uturuki:

Kusikiliza / IOM yapeleka msaada wa vifaa vya baridi kwa wakimbizi wa Syria

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepeleka misaada ya kibinadamu kwa ajili ya majira ya baridi kwa familia za wakimbizi wa Syria zaidi ya 3,160   kwenye mji wa  Kirikhan jimbo la  Hatay nchini Uturuki tangu wakati wa Krismasi ili kukabiliana na baridi kali na mazingira magumu wanayoishi. Familia hizo zenye watu jumla ya 16,370 zimepokea [...]

24/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashauriano na pande mbili za Syria yanatia moyo: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi, Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kwenye mzozo wa Syria

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Nchi za kiarabu kwenye mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi ameanza mazungumzo kwa nyakati tofauti na pande mbili zinazokinzana nchini humo huko Geneva, Uswisi ambapo amewaeleza waandishi wa habari kuwa mazungumzo hayo yamekuwa ya kutia moyo na yataendelea kesho. Bwana Brahimi amesema pande zote mbili [...]

24/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upatikanaji wa huduma ya maji safi waangaziwa nchini Tanzania

Kusikiliza / Mama akiteka maji

Ikiwa ni miezi miwili kabla ya dunia kuadhimisha siku ya maji duniani, wataalamu wamekuwa wakibonga bongo juu ya nini kufanya ili huduma hiyo adhimu iweze kuwafikia wananchi wengi bila gharama kubwa. Mathalani kongamano la Zaragoza huko Hispania lilifanyika kama maandalizi ya siku hiyo likimulika maudhui ambayo ni umuhimu wa maji na nishati na uhusiano kati [...]

24/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya machafuko WFP inaendelea kutoa msaada CAR:

Kusikiliza / Usambazaji wa chakula Bangui, WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaendelea kutoa msaada wa chakula kwa wakimbizi wa ndani katika mji mkuu Bangui  na miji mingine ya Bouar na Bossangoa licha ya machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Shirika hilo limeongeza kuwa usalama mdogo umesababisha maelfu ya watu kushindwa kurejea makwao na pia kuingilia shughuli [...]

24/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Athari za ghasia Sudan Kusini kwa familia moja

Kusikiliza / Mtoto Nyariek

Kufuatia ghasia zinazoendelea Sudani Kusini wanawake na watoto ndio wanaoathirika pakubwa na hivyo kumomonyoa familia kwa ujumla. Katika makala ifuatayo Grace Kaneiya anamulika kisa cha mtoto ambaye mama yake aliuliwa. Ni kisa chenye simanzi na kusisimua. Ungana naye.

24/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulio la kigaidi Misri

Kusikiliza / Ramana ya Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Maraifa leo amelaani shambulio la kigaidi mjini Cairo nchini Misri ambalo limesababisha vifo vya watu na kujeruhi watu kadhaa. Taarifa ya ofisi ya msemaji wa katibu mkuu iliyotolewa leo ijumaa mjini New York inasema Bwana Ban amesema hakuna sababu inayoweza kuhalalisha vitendo kaam hivyo vya kigaidi. Bwana Ban ametuma salamu [...]

24/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mradi wa ushirikiano wa nchi za Kusini kusaidia uhakika wa chakula Angola

Kusikiliza / Zaidi ya watafiti 100 wa Kilimo na Mifugo wa Angola kupata mafunzo nchini Brazil

Uhakika wa chakula nchiniAngolaambao umekuwa wa mashaka sasa umepatiwa shime kufuatia makubaliano ya mradi wa miaka miwili kati ya nchi hiyo naBrazilna ushirikiano wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO. Mradi huo wa miaka miwili unagharimiwa kwa pamoja na nchi mbili hizo kwa thamani ya Dola Milioni Mbili nukta Mbili ukiwa ni ushirikiano kati [...]

24/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lasifu makubaliano ya Sudan Kusini, lataka utekelezaji wa dhati

Kusikiliza / Mwananchi akipeperusha bendera ya Sudan Kusini

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameunga mkono hatua ya hivi karibuni zaidi ya pande mbili kinzani huko Sudan Kusini kutia saini mjiniAddis AbabaEthiopiamakubaliano ya kusitisha mapigano. Katika taarifa yao wametaka pande husika ambazo ni serikali na wafuasi wanaomuunga mkono makamu wa Rais wa zamani, kutekeleza kwa dhati kama hatua ya awali [...]

24/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamia ya mamilioni ya ekari za ardhi huenda zikaharibiwa ifikapo 2050: UNEP

Kusikiliza / Utengenezaji wa matofali ya kuchoma una manufaa lakini unasababisha ukataji miti ambao huharibu mazingira. (Picha-UNEP)

Ardhi ya asili yenye ukubwa wa ekari milioni 849 kote duniani, ambayo ni karibu sawa na eleo la ardhi nzima ya taifa la Brazil, huenda ikaharibiwa ifikapo mwaka 2050, ikiwa mienendo ya sasa ya matumizi ya ardhi yasiyo endelevu itaendelea, imeonya ripoti ya Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP. Katika ripoti [...]

24/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rasilimali watu yahitajika zaidi kukagua silaha za nyukilia Iran : IAEA

Kusikiliza / Yukia Amano

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA Yukiya Amano amesema wanahitaji kuongeza rasilimali watu ili waendane na ongezeko la kazi ya ukaguzi wa silaha za nyukilia nchini Iran. Bwana Amano ameiambia bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo  mjini Vienna, Austria kuwa  wakaguzi watahitaji kuyafikia maeneno zaidi na kwamba watahitaji kufunga vifaa [...]

24/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Usitishaji mapigano umekaribishwa Sudan Kusini lakini maelfu bado wanahitaji msaada

Kusikiliza / Mama na mwanawe ambaye alizaliwa chini ya mti wakati akikimbia kutoka Bor kuelekea Uganda

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamekaribisha utiaji saini hatua ya kusitisha mapigano baina ya serikali ya Sudan Kusini na majeshi ya waasi , lakini yanasema maelfu ya wakimbizi wa ndani bado wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu. Joseph Msami na maelezo zaidi (RIPOTI YA JOSEPH MSAMI) Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeelezea [...]

24/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila kupunguza kiwango cha joto, maendeleo endelevu ni ndoto: Ban

Kusikiliza / WEF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amehutubia kongamano la dunia kuhusu uchumi huko Davos Uswisi na kuonya kuwa bila kupunguza kiwango cha joto duniani, harakati za kutokomeza umaskini na kufikia maendeleo endelevu zitakabakia ndoto. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Bwana Ban ametumia maudhui ya kongamanohilokuhusu hali ya hewa, ukuaji na [...]

24/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yapambana na surua miongoni mwa wakimbizi wa Sudan kusini nchini Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi wa Suda Kusini waliokimbilia Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo Ijumaa limeanza kampeni kubwa ya chanjo Kaskazini mwa Uganda ili kuzuia kusambaa kwa surua miongoni mwa wakimbizi wa Sudan Kusini. Flora Nducha na maelezo kamili (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Wizara ya afya yaUgandaimethibitisha kuwepo kwa mlipuko wa surua miongoni mwa wakimbizi zaidi ya 59,000 wa [...]

24/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031