Nyumbani » 23/01/2014 Entries posted on “Januari 23rd, 2014”

Sudan Kusini wakubaliana kusitisha mapigano, Ban apongeza

Kusikiliza / Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini  yalisababisha maelfu kusaka hifadhi kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa

Hatimaye pande zinazopingana huko Sudan Kusini zimetia saini makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza nchini humo tarehe 15 Disemba mwaka  jana, hatua ambayo imekaribishwa vyema na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. Akizungumza mjini Davos wakati akiwa kwenye shughuli ya shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kuhusu kutokomeza njaa, Bwana Ban amesema habari [...]

23/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usafiri, swala muhimu katika kujiimarisha kwa taifa la Somalia

Kusikiliza / Adan Mohammed

Wakati taifa la Somalia likiendelea kujiimarisha kiusalama na kimaendeleo miundombinu ya usafiri ni suala muhimu katika kufikia hatua hiyo. Joseph Msami anamulika hali ya uwanja wa kimataifa wa ndege Kismayo mji ambao ni kitovu cha uchumi cha Somalia. Ungana naye katika makala ifuatayo.

23/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunaweza kufikia MDGs kuhusu afya katika siku 700: Ray Chambers

Kusikiliza / MDG'S

Wadau wanaopigia debe kufikia malengo ya maendeleo ya milenia kuhusu afya, wamewasilisha leo mkakati wa siku 700 wa kuwaokoa watoto milioni 2.2 kutokana na kifo, na hivyo kulifikia lengo la maendeleo ya milenia kuhusu afya ya mtoto ifikapo tarehe ya ukomo wake ya Disemba 31, mwaka 2015. Mkakati huo unaunga mkono mkakati wa Katibu Mkuu [...]

23/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza EU kwa hatua ya awali ya kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / SG-DAVOS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye yuko Uswisi kwa ziara ya kikazi hii leo amezungumza na waandishi wa habari huko Davos na kusema anatiwa sana moyo kuona suala la mabadiliko ya tabianchi yanapatiwa kipaumbele. Bwana Ban ametolea mfano Kamisheni ya Ulaya ambayo amesema imetangaza pendekezo la matamanio makubwa ya kupunguza viwango vya [...]

23/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laiomba jamii ya kimataifa iendelee kuisaidia Mali

Kusikiliza / Baraza la Usalama

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito kwa jamii ya kimataifa iendelee kuwasaidia watu na serikali ya Mali katika juhudi za kufikia amani, utulivu na maridhiano na maendeleo ya taifa hilo. Katika taarifa ilotolewa na rais wake, wanachama wa Baraza hilo wamesema wanaendelea kutilia mkazo masikitiko yao kuhusu hali inayotia wasiwasi katika [...]

23/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tarehe ya kusikiliza kesi dhidi ya Kenyatta huko ICC yasogezwa hadi itakapotangazwa

Kusikiliza / Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague, Uholanzi, imefuta hadi itakapotangazwa tena, tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi inayomkabili Uhuru Kenyatta, kesi ambayo ilikuwa ianze tarehe Tano mwezi  ujao. Hiyo ni kwa mujibu wa tangazo la lililotolewa leo na jopo la majaji wanaosikiliza sualahilolikiongozwa na Jaji Chile Eboe-Osuji. Taarifa hiyo imesema badala yake [...]

23/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka mauaji Myanmar yachunguzwe

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka serikali ya Myanmar kuchunguza matukio mawili kaskazini mwa jimbo la Rakhine katika kijiji kiitwacho Du Chee Yar Tan kati ya January 9 na 13 ambapo zaidi ya waislamu 40 wa Rohingya waliripotiwa kuuwawa. Bi Pillay amesema analaani upotevu wa maisha ya watu [...]

23/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kampeni maalum ya UM ya kuwafikia wasiofikika Syria yaonyesha mafanikio

Kusikiliza / Mitandao

  Kampeni ya siku tatu ya Umoja wa Mataifa isiyokuwa ya kawaida iliyohusisha mitandao ya kijamii ikiwamo twiter na face book imewafikia zaidi ya watu milioni 31 na wengine mamilioni wakipaza sauti zao kutaka pande zinazohusika na mgogoro nchini Syria kuruhusu  misaada iwafikie watu walioko Yarmouk eneo lililoko karibu naDamascusambako wakimbizi wa Palestina walioko Syria [...]

23/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lamulika hali Mali, Darfur na Sudan Kusini

Kusikiliza / Herve Ladsous

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo, limekutana kufanya mashauriano kuhusu hali nchini Mali, pamoja na kujadili hali katika eneo la Darfur, Sudan na hali nchini Sudan Kusini. Joshua Mmali na taarifa kamili. (TAARIFA YA JOSHUA) Baada ya kuridhia taarifa ya rais wa Baraza hilo kuhusu hali nchini Mali, wanachama wake wamemsikiliza Msaidizi wa [...]

23/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mratibu Maalum wa UM huko Lebanon atembelea Akkar

Kusikiliza / Derek Plumbly, mratibu maalum wa UM huko Lebanon akizungumza na mtoto kwenye moja ya maeneo yanahohifadhi wa wakimbizi wa Syria kaskazini mwa Lebanon

Eneo la Akkar kaskazini mwa Lebanon lilipata ugeni wa Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Derek Plumbly ambaye alifanya ziara kujionea hali  halisi ya wakimbizi wa Syria waliosaka hifadhi baada ya kukimbia mapigano nchini mwao. Alipata fursa ya kuzungumza na maafisa wa usalama mpakani, wawakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa ya kuhudumia [...]

23/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Raia wa Uingereza afukuzwa Uganda; Kisa mapenzi ya Jinsia moja

Kusikiliza / Bendera ya Uganda

Takribani mwezi mmoja baada ya Ofisi ya Haki ya Umoja wa Mataifa kueleza hofu yake juu ya kupitishwa kwa sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda, raia wa Uingereza, Bernard Randell amefukuzwa nchini humo baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye mapenzi hayo. Tayari Randell ameagizwa kuondoka nchini humo katika saa kumi na [...]

23/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Darfur changamoto ni nyingi lakini hatukati tamaa: Mkuu UNAMID

Kusikiliza / Mohamed Ibn Chambas, Mkuu wa UNAMID

Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur, UNAMID nchini Sudan Mohamed Ibn Chambas amezungumza na waandishi wa habari huko Khartoum akisema mwaka jana umeshuhudia ghasia zikishika kasi kwenye eneo hilo lakini ofisi yake haitokata tamaa ili kuendelea kuweka ulinzi na mustakhbali wa wakazi wa eneo [...]

23/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka uwekezaji uelekezwe kwa wasichana katika nchi zinazoendelea:

Kusikiliza / Wasichana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hivi sasa dunia inakimbizana na wakati zikiwa zimesalia zaidi ya siku 700 kabla ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015. Flora Nducha na maelezo zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Ban ameyasema hayo Alhamisi kwenye chakula cha mchana kuchagiza mafanikio ya malengo ya maendeleo ya [...]

23/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunajitahidi kuongeza operesheni zetu pale panapowezekana:WFP

Kusikiliza / WFP yaongeza operesheni Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza operesheni kubwa ya dharura ili kuwafikishia chakula maelfu ya watu wanaokimbia mapigano katika taifa jipya kabisa la Sudan Kusini. Ukosefu wa usalama unamaanisha kwamba kuwafikishia chakula wmaelfu ya watu wenye njaa ni changamoto, lakini hata hivyo tangu kuzuka kwa machafuko WFP imeweza kuwafikia watu 178,000 wanaohitaji msaada. [...]

23/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tume ya fidia ya UM yalipa dola bilioni 1.3

Kusikiliza / Nembo ya UN

Tume ya fidia ya Umoja wa Mataifa Alhamisi imelipa dola bilioni 1.03 kwa serikali yaKuwaitikiwa ni deni lililosalia kwa nchi hiyo kwa ajili ya kuwalipa waathirika fidia. Tume ya fidia ya Umoja wa Mataifa ilianzishwa mwaka 1991 kufuatia azimio la baraza la usalama namba 687 na 692 lililotaka kushughulikiwa kwa madai na kulipa fidia kwa [...]

23/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031