Nyumbani » 22/01/2014 Entries posted on “Januari 22nd, 2014”

Ban atangaza tume ya kuchunguza matukio CAR tangu Januari 1 2013

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametangaza tume ya uchunguzi katika matukio nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu Januari 1 mwaka 2013, kufuatia ombi lililotolewa na Baraza la Usalama kwamba tume hiyo iundwe, katika azimio lake 2127(2013) la Disemba 5, 2013. Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa Jumatano jioni na msemaji wa Katubu [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laelezwa kuhusu ubakaji na hatari ya mauaji ya kimbari CAR

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakinyoosha mkono kupiga kura

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng, ameliambia Baraza la Usalama leo kuwa licha juhudi zilizofanywa na viongozi wa kidini kama kasisi na Imam wa mji wa Bangui kuendeleza amani na mazungumzo, ni mafanikio machache sana yaliyopatikana. Akilihutubia Baraza hilo ambalo limekutana kujadili hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakenya waliokimbilia Uganda baada ya uchaguzi mwaka 2007 hawakurudi makwao

Kusikiliza / Wakenya waliokimbilia nchi jirani Uganda baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007

Uchaguzi tata wa mwaka 2007 nchini Kenya ambao ulipelekea kuzuka kwa ghasia baada ya matokeo kutangazwa ulichangia wananchi wengi kukimbilia nchi jirani ili kuepuka ghasia. Miaka 6 baadaye bado kuna wakimbizi wengi walioko nchi jirani waliko tafuta hifadhi ikiwemo Uganda. ijapokua wana nia ya kurudi nyumbani lakini bado wanahofia kama watarudi wapi basi ungana na [...]

22/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati za UNICEF kukabili utapiamlo Sudan zaungwa mkono

Kusikiliza / Mtoto akipimwa iwapo ana utapiamlo huko Darfur, Sudan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF litapokoea Euro Milioni Mbili kutoka Ofisi ya usaidizi wa kibinadamu ya Tume ya  Ulaya kwa lengo la kuimarisha harakati za kupambana na utapiamlo nchiniSudan. Mwakilishi wa UNICEF huko Sudan Geert Cappelaere amesema uhai wa mtoto nchini humo unakabiliwa na vitisho kadhaa ikiwemo utapiamlo na kwamba watoto [...]

22/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya hali ya hewa ni ajenda kuu kwenye kongamano la dunia la uchumi Davos:

Kusikiliza / Nembo

Mabadiliko ya hali ya hewa yamepangwa kuwa ajenda kuu katika kongamano la kimataifa la uchumi linaloendelea huko Uswizi. Zaidi ya viongozi 2500 kutoka nchi takriban 100 wakiwemo wakuu wa nchi  na serikali zaidi ya 30 wanatarajiwa kushiriki kwenye siku nne za kongamano la kimataifa la uchumi mjini Davos. Wawakilishi wa kutoka sekta za umma, binafsi [...]

22/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Montreux umekuwa wa mafanikio, sasa kazi kubwa inaanza Ijumaa: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati wa kuchukua hatua za kijasiri ni sasa ili kumaliza madhila yanayokumba wananchi waSyria, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon huko Montreux, Uswisi baada ya mkutano wa ngazi ya juu wa kuonyesha mshikamano na Syria. Bwana Ban amewaeleza waandishi wa habari kuwa mkutano huo ulikuwa wa mafanikio makubwa kwani kwa mara ya [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yazindua mfumo mpya wa Usajili kambini:Malawi

Kusikiliza / Mtoto wa kike afanyiwa upelelezi katika kambi ya Dzaleka, UNHCR

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, limehitimisha jaribio la kwanza la mfumo mpya ambao unaotarajiwa kulisaidia kusajili na kulinda watu kwa njia bora zaidi. Mfumo huo utasaidia kuhakiki vitambulisho na misaada wanayohitaji watu walolazimika kuhama katika operesheni za UNHCR kote duniani. Grace Kaneiya na maelezo zaidi  (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Zoezi la [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pande mbili husika, mzozo wa Syria zakutana ana kwa ana Uswizi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati wa kongamano Uswizi

Kongamano la kimataifa linalolenga kuumaliza mzozo uliopo nchini Syria umefunguliwa leo mjini Montreux Uswisi leo Jumatano huku wito ukitolewa kwa pande zote kujitoa kwa mazungumzo yakinifu ili kumaliza takriban miaka mitatu ya ghasia. George Njogopa na taarifa kamili  (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameelezea mapigano yanayoendelea nchini Syria kama vita vilivyopindukia ambavyo [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Syria na Upinzani jukwaani

Kusikiliza / Wakati wa mkutano

Kongamano la Montreux limehutubiwa na wawakilishi wa Marekani, Urusi, serikali ya Syria na upinzani. Mwakilishi wa serikali ya Syria alikuwa ni Waziri wake wa Mambo ya Nje, Walid al-Moallem ambaye amesema baadhi ya watu walioko kwenye kongamanohilowalijaribu kuirejesha nchi yake katika enzi za zamani, huku akitaja baadhi ya maovu yanayotekelezwa nchiniSyria.  (SAUTI YA Walid Al- [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakuu wa mashirika ya misaada ya UM watoa wito wa kuwalinda watoto Syria

Kusikiliza / Watoto wa Syria

Viongozi wa mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa mataifa na askofu mkuu Desmond Tutu wametoa wito kwa pande zote nchini Syria zinazokutana Switzerland kuchukua hatua ya haraka kuwalinda watoto nchini Syria. Katika baruayaoiliyoandikwa kabla ya mkutano ulianza leo Jumatano, Montreux  wakisema zaidi ya watoto 11,000 wa Kisyria wameshapoteza maisha yao. Kuanzia makombora yanayovurumishwa [...]

22/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mradi maalumu wazinduliwa kuzuia tatizo la kudumaa Malawi:WFP

Kusikiliza / Mtoto

Mradi mpya wenye nia ya kupambana na tatizo la kudumaa umezinduliwa leo Jumatano nchini Malawi limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Kutokuwepo kwa usalama wa chakula mara kwa mara, lishe duni na kujirudia kwa maradhi ni miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha kudumaa, miongoni mwa karibu watoto milioni moja wa Malawi walio chini ya [...]

22/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tamko la Geneva ndio msingi wa hatma ya Syria; Marekani, Urusi

Kusikiliza / John Kerry, Waziri wa Mambo  ya nje wa Marekani akizungumza kwenye mkutano kuhusu Syria huko Montreux, Uswisi

Marekani na Urusi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kufanikisha mkutano wa kimataifa wa amani kuhusu Syria, zimesema mashauriano ya Montreux nchini Uswisi yaliyotangulia mkutano huo utakaofanyika Ijumaa, ni fursa pekee ya kuleta amani ya kudumu. Wajumbe wa pande hizo wakizungumza wakati wa ufunguzi wa mashauriano hayo yaliyolenga kuonyesha mshikamano na Syria wamesema wakati ni huu [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano huu ni lazima utoe matumaini ya hatma ya Syria:OIC

Kusikiliza / Katibu mkuu wa OIC, Iyad Amin Madani,

Jumuiya ya nchi za Kiislam OIC ambayo inahudhuria mkutano kuhusu Syria imesema inaamini mkutano huo ni lazima uumalize machafuko yanayoendelea Syria  Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) OIC imeongeza kuwa mkutano wa leo ni lazima uhakikisha Syria inajikita katika mustakhbali wenye matumaini, uhuru, usawa, na kuheshimu haki za binadamu kwa Wasyria wote [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutokomeza njaa ni jukumu la kila mtu: WFP

Kusikiliza / Nembo

Kongamano la uchumi duniani limeanza leo Jumatano  huko Davos, Uswisi ambapo Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linatumia mkutano huo kuweka bayana ujumbe ya kwamba suala la kutokomeza njaa ni jukumu la kila mtu. Mkurugenzi Mkuu wa WFP Ertharin Cousin ataungana na wabia wengine kushawishi ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma [...]

22/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Surua yatishia uhai wa watoto nchini Guinea: UNICEF

Kusikiliza / Watoto wasubiri kuchanjwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na wadau wake wameanza maandalizi ya kampeni ya kuwapatia chanjo dhidi ya Surua watoto zaidi ya Milioni Moja nukta Sita nchini Guinea ili kuepusha mlipuko wa ugonjwa huo hususan mji mkuu Conakry. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Mwakilishi wa UNICEF nchini humo [...]

22/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031