Nyumbani » 21/01/2014 Entries posted on “Januari 21st, 2014”

Ban asikitishwa na shambulio la bomu Lebanon

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari kusini mwa mji wa Beirut katika mtaa wa makazi na biashara uitwao Haret Hreik na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa. Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kwa waathirika wa tukio hilo na kwa serikali na watu wa Lebanon na kutaka [...]

21/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban awa na mazungumzo na Dkt. Elaraby huko Geneva

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu Dkt. Nabil Elaraby

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye yuko Geneva Uswisi kwa shughuli kadhaa ikiwemo kushiriki mazungumzo ya kimataifa ya amani kuhusuSyria, amekuwa na mashauriano na Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu, Dkt. Nabil Elaraby. Wawili hao wamejadili mazungumzo ya ngazi ya juu ya kuonyesha mshikamano naSyria  yatakayofanyika kesho Jumatano huko Montreaux, [...]

21/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa Syria unachangia raia wa nchi hiyo kukimbilia nchi jirani Iran

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria watafuta hifadhi Iran

Wakati mzozo wa Syria ukiendelea kutawala katika vichwa vya habari kote duniani,huku suluhu la kisiasa ikiwa ndio mchakato unaondelea hivi sasa, wakimbizi raia wa Syria wanaendelea kuhaha kutafuta hifadhi huku wakikumbana na mikasa mbalimbali. Nchini Iraq nchi inayotajwa kuwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, hilo haliwazuii wakimbizi wa Syria kujihifadhi humo, baada ya mpka [...]

21/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waongeza misaada kuwafikia manusura wa mapigano Iraq

Kusikiliza / Ramana ya Iraq

Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watu waliopoteza makazi na familia kadhaa kushikiliwa kutokana na mapigano yanayoendelea katika miji tofauti jimboni Anbar nchini Iraq Umoja wa Mataifa umeongeza misaada ya kiutu ili kuzinusuru jamii hizo. Mathalani hadi January 20 zaidi ya familia 22,000 zimejiandikisha kama wakimbizi wa ndani wengi wao wakiwa jimboni Anbar na maeneo mengine [...]

21/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mfumo mpya wa matumizi ya mazao ya baharini wahitajika: FAO

Kusikiliza / Uvuvi wa kupindukia huhatarisha uwepo wa samaki na uhakika wa chakula

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amesema mabadiliko makubwa yanahitajika kufanyika kwenye matumizi ya mazao ya baharini ili kuweka uhakika wa chakula na ustawi wa maeneo ya pwani  na nchi za visiwani. Akizungumza hukoAbu Dhabi, Bwana Da Silva amesema dunia haiwezi kuendelea kutumia rasilimali za bahari na [...]

21/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalamu muhimu wa UM wataka mkutano wa Geneva II kufikia muafaka wa amani:

Kusikiliza / Nembo ya UM

Kundi la wawakilishi ambao ni wataalamu wa masuala ya haki za binadamu kwenye mfumo wa Umoja wa mataifa wametoa wito kwa mkutano ujao wa Syria, Geneva II kuafikiana kuhusu hatua za kumaliza machafuko kwa amani. Katika barua yao ya wazi iliyochapishwa leo Jumanne wataalamu hao pia wametaka kuwe na lengo na wajibu wa amani ya [...]

21/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu ya usalama yatishia wananchi kurejea Bangui: IOM

Kusikiliza / Watu wa CAR Warudishwa nyumbani wanopewa kipaumbele ni wanawake na walio na mahitaji ya kiafya

Idadi kubwa ya watu waliosaka hifadhi kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui na viunga vyake wamelieleza shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kuwa hofu ya usalama ni sababu kuu ya wao kugoma kurejea makwao. Katika utafiti huo wa kwanza ulioendeshwa na IOM kwa ushirikiano na wadau wake kwenye maeneo 46 mjini [...]

21/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ndege ya kwanza ya UNICEF yawasili Juba kunusuru afya za wanawake na watoto.

Kusikiliza / UNICEF Sudan Kusini wakitoa maelezo kwa familia

Ndege ndogo ya kwanza miongoni mwa ndege mbili za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, ikiwa na tani 35 za misaada ya dharura nchini Sudan Kusini zimewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba . Grace Kaneiya na maelezo zaidi (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Ndege hiyo imebeba vifaa vya tiba kwa [...]

21/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR na serikali ya Uganda wafungua upya kambi kwa ajili ya wakimbizi

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini kambini

Nchini Uganda, kambi ya wakimbizi ya Nyumanzi na ile ya Paratuku zilizo kaskazini mwa nchi hiyo zimefunguliwa upya ili kupatia makazi raia wa Sudan Kusini wanaokimbia vita nchini mwao. Kwa sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na serikali ya Uganda wanashirikia kuimarisha kambi hizo kwani tangu mwezi uliopita idadi ya wakimbizi [...]

21/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Plumbly alaani shambulio la bomu kusini mwa Beirut

Kusikiliza / Derek Plumbly

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Derek Plumbly, amelaani vikali shambulizi la bomu lililochukuliwa kwa gari leo asubuhi kwenye mtaa wa makazi na biashara wa Haret Hreik kusini mwa Beirut, na ambalo limewaua watu kadhaa na na kuwajeruhi wengine. Ametuma risala za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo Plumbly amesema, shambulio [...]

21/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM Uganda inachagiza kampeni dhidi ya ukimwi miongoni mwa wasafiri

Kusikiliza / IOM linagawa vifaa vya maabara na tiba nchini Uganda

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linagawa vifaa vya tiba na maabara katika vituo mbalimbali vya afya nchini Uganda hasa katika maeneo yenye maambukizi makubwa ya HIV ili kukabiliana na maambukizi hayo katika maeneo makubwa ya usafiri. HIV na ukimwi bado unanyanyapaliwa nchiniUgandana hususani katika jamii za uvuvi amesema Salongo Dennis Lukyamuzi mmoja wa wavuvi [...]

21/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sheria mpya Ukraine huenda zikaathiri vibaya mno haki za binadamu: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameelezea kusikitishwa na sheria ilopitishwa mnanmo Alhamis wiki ilopita, ambayo inaweka masharti makali katika kufurahia haki za binadamu za msingi, zikiwemo haki na uhuru wa kujumuika na kujieleza, na kuweka adhabu kwa wanaozikiuka, ikiwemo kufungwa jela. Bi Pillay amesisitiza haja ya kuwepo mazungumzo [...]

21/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Silaha za Kemikali Syria ni ukumbusho wa haja ya kuzitokomeza: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa kamati kuhusu utokomezaji wa silaha kufanya juhudi ili kuondoa mkwamo uliopo kwa mpango wake wa kuchukua hatua. Bwana Ban amesema matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria yalikuwa ukumbusho wa haja ya kukabiliana na hatari zinazoletwa na silaha zote za mauaji ya [...]

21/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031