Nyumbani » 17/01/2014 Entries posted on “Januari 17th, 2014”

Shambulio Kabul lasababisha vifo vya watu 14; Ban, Baraza la Usalama walaani vikali

Kusikiliza / Makao Makuu ya UNAMA mjini Kabul, Afghanistan. (Picha-UNAMA)

Nchini Afghanistan, watu 14 wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa kufuatia shambulio la Ijumaa kwenye mgahawa mmoja katikati mwa mji mkuu Kabul. Miongoni mwa waliouawa ni raia wa nchi hiyo na wa kigeni wakiwemo wafanyakazi wanne wa Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameshutumu vikali shambulio hilo na kusema kuwa matukio [...]

17/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kundi la maigizo la IOM laanza ziara yake vijijini huko Ethiopia

Kusikiliza / Raia wa Ethiopia waliokuwa wanaishi Saudi Arabia wakifuata taratibu ya usajili ili kurejea nyumbani

Kikundi mashuhuri cha michezo ya kuigiza kinachoratibiwa na Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kimeanza ziara yake vijijini nchiniEthiopiaikilenga zaidi maeneo yenye wahamiaji wasio halali huko Amhara, Tigray na Oromia. Idadi ya raia waEthiopiawanaorejea nyumbani kutokaSaudi Arabiaambako walikuwa wanaishi bila vibali imeongezeka na kufikia 154,000 na hivyo maigizo hayo yanalenga kuelimisha madhila ya kuishi ugenini [...]

17/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Myanmar ichunguze mapigano kati ya jeshi dhidi ya waislamu

Kusikiliza / Tomás Ojea Quintana, mtalaam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini yanmar

Mtalaam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu huko Myanmar, Tomás Ojea Quintana ameitaka serikali ya nchi hiyo kuchunguza ripoti za mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na waumini wa kibuda na kiislamu kwenye jimbo la Rakhine. Mapigano hayo yaliyotokea kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita yamedaiwa kusababisha zaidi ya watu Laki [...]

17/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kongamano la wiki ijayo ni muhimu katika kutafuta suluhu kwa mzozo Syria:Ban

Kusikiliza / Mkimbizi wa Syria na wanawe katika kambi ilioko Lebanon. Wanakabiliwa na mahitaji kama mamilioni ya wengine

Kongamano la kimataifa kuhusu harakati za amani nchini Syria, linatazamiwa kuanza wiki ijayo mnamo tarehe 20 Januari. Kongamano hilo ambalo kuwepo kwake kumekumbana na changamoto nyingi, linatarajiwa kutoa nafasi muhimu ya kupata suluhu la kisiasa kwa mzozo wa Syria, ambao umekuwa ukitokota kwa miaka mitatu sasa. Baada ya muda mrefu wa kujaribu kuzishawishi pande zinazozozana [...]

17/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Zana za kilimo zaleta mapinduzi ya kilimo duniani.

Kusikiliza / Kilimo cha kisasa

   Zana za kisasa za kilimo zimehuisha kilimo husuani barani Afrika na hivyo kupunguza adha za mamilioni ya familia za wakulima duniani  barani humo limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Kwa mujibu wa chapisho la FAO lenye jina zana za kilimo kwa ajili maendeleo vijiini, mapitio ya mifumo na maendeleo duniani, ukuaji usiokwepeka wa [...]

17/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Gharama kubwa ya mishahara ya watumishi serikalini Zambia yatishia uchumi: IMF

Kusikiliza / kwacha

Shirika la fedha duniani, IMF limesema mafanikio ya kiuchumi yaliyokuwepo nchini Zambia yanakabiliwa na changamoto kubwa ya nakisi ya fedha. Mkuu wa IFM nchini humo John Wakeman-Linn amesema serikali ya Zambia inatumia fedha nyingi zaidi kuliko inazokusanya kwenye kodi na hivyo kutishia uchumi. Mathalani ametaja gharama ya mishahara kwa watumishi wa serikali ambayo ni asilimia [...]

17/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO yataja hatua muhimu za kupiga vita njaa na utapiamlo

Kusikiliza / Kilimo bora ni muhimu kuepusha mazao kushambuliwa na wadudu na hatimaye kusababisha njaa. (Picha-FAO)

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema kuweka mifumo chakula ambayo inazingatia afya na endelevu ni mojawapo ya njia sahihi za kupiga vita njaa na  utapiamlo duniani. Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FAO Helena  Semedo huko Berlin Ujerumani wakati wa mkutano wa imataifa wa chakula na kilimo kwa mwaka huu wa 2014. [...]

17/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Alshabaab watangaza marufuku ya kutumia internet Somalia, wananchi walalama!

Kusikiliza / Internet nchini Somalia

Wakati taifa la Somalia likjitutumua katika ustawi wake kiuchumi, kisiasa na kijamii, juhudi hizo zinakumbana na vikwazo mbalimbali ikiwamo tishio la usalama wa mawasiliano kimtandao. Hapa namaanisha mtandao wa internet . Katika hali ya kushangaza  kundi la kigaidi la Al shabaab ambalo limekuwa linahatarisha usalama nchini humo limepiga marufuku wananchi kutumia mtandao wa internet. Hi [...]

17/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wetu ni silaha thabiti ya kukabiliana na majanga yanayoendelea: Ban

Kusikiliza / Mfanyakazi wa UNHCR akiwa ametembelea moja ya familia kutoka Mali iliyosaka hifadhi huko Burkina Faso

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limehutubiwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akiangazia zaidi hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Umoja huo kwenye mizozo ya Syria, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na ile ya demokrasia ya Congo, DRC ambapo ametaka viongozi kuweka kando maslahi ya kitaifa na badala yake kushirikiana kwa pamoja na kumaliza [...]

17/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

CERF yatenga dola Milioni 86 kusaidia nchi 10 zenye majanga mabaya zaidi.

Kusikiliza / CERF husaidia watoto kwenye maeneo ya majanga kuwa na uhakika wa mlo

Mratibu Mkuu wa usaidizi wa kibinadamu ndani ya Umoja  wa Mataiaf Valerie Amos ametenga dola Milioni 86 kwa ajili ya operesheni za usaidizi za Umoja huo kwenye maeneo yenye majanga makubwa zaidi na ambayo pia yamesahaulika. Fedha hizo zinatoka mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia majanga, CERF na zinaelekezwa nchi kumi ambazo ni [...]

17/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yahitaji fedha zaidi kunusuru mahitaji ya chakula CAR

Kusikiliza / Afisa wa WFP akishuhudia watoto wakiandaa mlo huko CAR

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema linakabiliwa na upungufu wa fedha kwa ajili ya kugawa mahitaji ya chakula nchini jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Shirika hilo linasema ili kuepuka kugawa nusu chakula kwa walengwa au kuahirisha kabisa ahadi zaidi za fedha zinahitajika wakati huu ambapo uhaba wa chakula ni dhahiri. Kwa sasa [...]

17/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utawala wa Sheria waweza kuwa kichochezi cha fursa jumuishi za maendeleo: Eliasson

Kusikiliza / Jan Eliasson, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Hii leo kwenye Umoja wa Mataifa, umefanyika mdahalo kuhusu utawala wa sheria na jinsi unavyoweza kuwa kichochezi cha fursa jumuishi za maendeleo. Mdahalo huo umefanyika kabla ya mazungumzo ya kamati ya kuchukua hatua kuhusu malengo ya maendeleo endelevu. Mdahalo huo umefanyika ili kuangalia jinsi ujumuishaji wa suala la utawala wa sheria katika ajenda ya maendeleo [...]

17/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aweka matumaini ya Syria huko Geneva, kambi ya Yarmouk yapaziwa sauti

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Wakati macho na masikio yataelekezwa huko Uswisi wiki ijayo kwenye mkutano wa pili wa kimataifa juu ya amani ya Syria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema tukio hilo ni fursa pekee ya kuleta amani nchini humo. Amekaririwa akisema ni matumaini yake pia suala la mamlaka za mpito litatekelezwa kwa mujibu wa makubaliano [...]

17/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nilichoshuhudia Sudan Kusini kinatisha: Šimonović

Kusikiliza / Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya haki za binadamu, Ivan Šimonović akiwa kwenye moja ya kambi huko Sudan Kusini

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya haki za binadamu, Ivan Šimonović amehitimisha ziara yake ya siku nne huko Sudan Kusini na kusema kwa ujumla hali inatisha na pande zote kwenye mzozo huo zimefanya mauaji ya kutisha. Akizungumza mjini Juba, Šimonović amesema ziara yake ilimpeleka Juba mji mkuu wa Sudan Kusini, [...]

17/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatafuta kambi zaidi Afrika Mashariki kwa wakimbizi wa sudani Kusini

Kusikiliza / Kambi ya wakimbizi wa Sudan Kusini

Idadi ya wakimbizi wa Sudani Kusini wanaovuka mpaka kuelekea nchi jirani inatarajiwa kufikia laki moja mwishoni mw amwezi January kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbiozi UNHCR.Taarifa zadi na Joseph Msami  (TAARIFA YA MSAMI) Tangu katikati ya mwezi December mgogoro nchini humo ulipoanza zaidi ya raia elfu 86 wa Sudani Kusini wamevuka [...]

17/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto 6000 wametumikishwa jeshini CAR, miongoni mwao ni wa kike

Kusikiliza / Mtoto aliye na silaha

Idadi ya watoto waliotumikishwa kwenye vikundi vyenye silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati inaweza kufikia Elfu Sita, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF. Grace Kaneyia na ripoti kamili.  (Ripoti ya Grace)  UNICEF inasema ghasia na ukosefu wa usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati vimesababisha [...]

17/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031