Nyumbani » 16/01/2014 Entries posted on “Januari 16th, 2014”

Wajasiriamali Zimbabwe sasa kuuza bidhaa zao Ulaya kirahisi

Kusikiliza / SMEs

Wajasiriamali wa kati na wadogo (SMEs) nchini Zimbabwe huenda wakaanza kushuhudia bidhaa zao zikipata soko Ulaya kufuatia makubaliano ya ufadhili wa kifedha kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na kituo cha kimataifa cha biashra (ITC) wa zaidi ya uero milioni mbili katika mpango wa kuimarisha mazingira ya kibiashara ya nchi hiyo. Ufadhili huu unaosimamiwa na [...]

16/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka masuala muhimu ya mzozo wa Mali yashughulikiwe

Kusikiliza / baraza-la-usalama3-300x257

Wanachama wa Baraza la Usalama wamekaribisha kufanyika kwa uchaguzi wa urais na ubunge hivi karibuni nchini Mali, kama hatua muhimu ya kurejesha uongozi wa kikatiba nchini humo. Wanachama hao ambao wamesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu ilowasilishwa na Mwakilishi wake nchini Mali, Albert Koenders, wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza harakati jumuishi za kisiasa, ambazo zitaleta maridhiano na [...]

16/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Licha ya mapigano, wanafunzi wafanya mitihani Sudani Kusini!

Kusikiliza / Wanafunzi Sudani Kusini

Si rahisi kufikiria kwamba katikati ya mizozo watu wanaweza kupata elimu! Lakini hilo limetokea huko Sudani Kusini ambapo licha ya mapigano ya kikabila yanayoendelea nchini humo, wanafunzi wa shule ya msingi wanafanya mitihani ya kuhitimisha elimu ya msingi. Lakini mtihani huo unafanyika tofauti na walivyozoea, chini ya ulinzi mkali wa polisi. Ungana na Joseph Msami [...]

16/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Waathirika wa kimbunga nchini Ufilipino bado wanahitaji misaada.

Kusikiliza / Baada ya Kimbunga Haiyan Ufilipino

Miezi miwili baada ya kimbunga Typhoon Haiyan kuikumba Ufilipino hatua kubwa zimechukuliwa katika maeneo mengi katika kujikwamua baada ya janga hilo la asili lakini bado watu wanategemea misaada ya kiutu hususani katika kujenga upya makazi yao, amesema mkuu wa shirika la kuratibu misaada ya kiutu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos Bi Amos amesema [...]

16/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Juhudi zaidi zahitajika kukabiliana na ulanguzi wa madawa na uraibu: UNODC

Kusikiliza / mmea wa afyuni

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi inayohusika na madawa na uhalifu, Yuru Fedotov, amesema kuwa biashara haramu katika dawa za kulevya ni tishio kubwa kwa afya ya umma, uongozi mzuri na maendeleo endelevu magharibi na kati mwa bara Asia, na kwingineko duniani. Bwana Fedeotov amesema hayo wakati akikutana na Waziri wa Afghanistan anayehusika na kukabiliana na [...]

16/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Virusi vya kidingapopo aina ya 3 vyaibuka tena kusini mwa Pacific

Kusikiliza / Nembo ya WHO

Virusi vya homa ya kidingapopo aina ya 3 vimeibuka tena katika nchi kadhaa za Kusini mwa Pacific baada ya karibu miongo miwili. Idadi ya visa inatarajiwa kuendelea katika miezi ijayo kwenye maeneo mengi ikiwemo kuongezeka Fiji, French Polynesia na Kiribati, wakati mlipuko mkubwa kwenye visiwa vya Solomon unamalizika. Hivi sasa wizara za afya za mataifa [...]

16/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali nchini Mali

Kusikiliza / Wakati wa kikao cha leo cha Baraza la Usalama kuhusu Mali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali nchini Mali, ambapo pia limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali nchini humo. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA) Akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu kwenye Baraza la Usalama, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Mali na Mkuu wa ujumbe wa kuweka utulivu [...]

16/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kemikali za sumu kutoka Syria kuhamishiwa kwenye meli ya kimarekani huko Italia.

Kusikiliza / Meli ya kimarekani, Cape Ray ambako kemikali zitahamishiwa. (Picha-OPCW)

Serikali ya Italia imekubali bandari yake ya Gioia Tuaro iliyoko bahari ya Mediterranean kutumika wakati wa zoezi la kuhamisha kemikali za sumu kali zaidi kutoka kwenye meli za mizigo na kuzipakia kwenye meli ya kimarekani, MV Cape Ray. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la kupinga kemikali za sumu, OPCW, Balozi Ahmet Üzümcü,  amethibitisha hayo [...]

16/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu maalum wa UM kuhusu haki za mjumuiko wa amani kuzuru Rwanda.

Kusikiliza / Maina Kiai, Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za mjumuiko wa amani

Maina Kiai, mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kujumuika kwa amani atakuwa na ziara rasmi nchini Rwanda kuanzia tarehe 20 mwezi huu. Hii ni ziara ya kwanza ya Bwana Kiai nchiniRwandaakiwa mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ambapo amesema haki za uhuru wa kujumuika ni misingi ya demokrasia na kwamba baraza la haki [...]

16/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yalemewa na wingi wa wakimbizi wa Sudani Kusini wanaomiminika Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini waliokimbilia nchini Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), na wadau wake nchini Uganda,  wanakumbana na changamoto mbalimbali kufuatia  kumiminika kwa wakimbizi kutoka Sudan Kusini.Ripoti ya hivi punde inasema, angalau wakimbizi elfu moja wanaingia nchini Humo kila siku. John Kibego wa radio washirika  Spice FM,Ugandana maelezo kamili  (Tarifa ya John Kibego) Idadi ya wakimbizi hapaUgandaimefikia 45,000 [...]

16/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Brahimi asikitishwa na NCC kujitoa kwenye ujumbe wa upinzani

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Mwakilishi maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kwenye mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi ameeleza masikitiko yake kufuatia hatua ya kikundi cha National Coordination Committee, NCC kujitoa katika ujumbe wa upande wa upinzani utakaoshiriki mkutano wa kimataifa wa amani kuhusu Syria wiki ijayo huko Uswisi. Ameelezea hayo wakati wa [...]

16/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

unyanyasaji wa watoto kingono katika kanisa usio wa haki: VATICAN:

Kusikiliza / Papa Francis

Uongozi waVatican umekuwa ukitetea jinsi unavyoshughulikia kashifa ya unyanyasaji wa watoto kingono unaofanywa na Mapadri wa kanisa Katoliki mbele ya kamati ya Umoja wa mataifa ya haki za mtoto, CRC. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Mwakilishi wa Vatican Geneva Askofu mkuu Silvano Tomasi ameiambia kamati kwamba kanisa Katoliki inapinga jaribio lolote [...]

16/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya kimbari CAR yananukia; lawama ni kwa jumuiya ya kimataifa: Ging

Kusikiliza / Moja ya familia iliyosaka hifadhi kwenye mji mkuu Bangui

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu imeonya kuwa kinachoendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kinaweza kuibua mauaji ya kimbari. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) John Ging, Mkuu wa operesheni wa OCHA amefanya ziara ya siku tano huko  Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyompatia fursa ya kutembelea miji [...]

16/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ndege ya Monusco yapata ajali Goma

Kusikiliza / Ndege zisizo na rubani yaani drones

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC umethibitisha kuanguka kwa ndege yake isiyo na rubani katika uwanja wa kimataifa wa Goma. Msemaji wa MONUSCO Kanali Felix Bass amesema licha ya kuharibika vibaya kwa ndege hiyo lakini haikusababisha madhara yoyote kwa binadamu. Kutoka huko Goma Desire Kanyama wa radio washirika Okapi [...]

16/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM washutumu makundi ya wanamgambo Syria kutekeleza mauaji ya halaiki

Kusikiliza / Kando na mauaji ya watu mzozo unachangia katika uharibifu wa mali Syria

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inashutumu makundi ya wanamgambo yanayoendesha shughuli zao ndani ya Syria kutekeleza mauaji ya umati wa raia na wafungwa inaowashikilia. Flora Nducha na habari kamili  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Ofisi ya haki za binadamu inasema imepokea taarifa za mfululizo wa mauaji ya umati wa raia na wapiganaji [...]

16/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu walaani mauaji ya mtu wao Syria

Kusikiliza / Nembo

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu wamekasirishwa na kifo cha mfanyakazi wa kujitolea wa shirika la mwezi mwekundu la Syria bwana Hekmat Mohamad Kerbaj, katika tawi lake la Dumair nje kidogo ya mji mkuu Damascus. Mfanyakazi huyo alifariki dunia tarehe 8 Januari baada ya mateso ya miezi 5 aliyokuwa ametoweka [...]

16/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930