Nyumbani » 15/01/2014 Entries posted on “Januari 15th, 2014”

Ban afanya mikutano na viongozi kadhaa pembezoni mwa kongamano la Kuwait

Kusikiliza / Wakakti wa mkutano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekutana na kufanya mazungumzo na maafisa wa Kuwait, wakiwemo mfalme wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al Sabah, Waziri Mkuu Sheikh Jaber Mubarak Al-Hamad Al-Sabah, na Naibu Waziri Mkuu Sheikh Sabah Khaled Al-Hamd Al-Sabah, pembezoni mwa kongamano la pili la kutoa ahadi za ufadhili wa kibinadamu kwa [...]

15/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Niliyoshuhudia Sudan Kusini ni mambo ya kutisha: Šimonovic

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani kwenye kambi ndani ya UNMISS huko Bentiu wakisaka huduma ya maji

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya haki za binadamu, Ivan Šimonovic ambaye yuko ziarani nchini Sudan Kusini, ametembelea Bentiu, mji mkuu wa   jimbo la Unity na kusema alichoshuhudia ni jambo la kusikitisha. Akizungumza akiwa kwenye moja ya kambi za wakimbizi wa ndani kwenye ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa [...]

15/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Haiti yaadhimisha miaka minne tangu ikumbwe na tetemeko la ardhi

Kusikiliza / Kumbukumbu ya tetemeko Haiti

Ni tukio lenye hisia na majonzi, ni tukio linalokumbusha vifo visivyotarajiwa. Pia tukio hili linakumbusha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya nchi. Hii ni Haiti inayoadhimisha miaka minne tangu tetemeko la ardhi liipige na kusababisha maafa . Ungana na Grace Kaneiya katika ripoti ifuatayo.

15/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na sheria ya kupinga ndoa za jinsia moja Nigeria

Kusikiliza / Mwanaharakati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameungana na mkuu wa haki za binadamu katika umoja huo Navi Pillay katika kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya serikali ya Nigeria kutia saini sheria ya kupinga ndoa za jinsia moja. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa katibu mkuu leo mjini New York, [...]

15/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya dola Bilioni 2.4 zaahidiwa ili kuikwamua Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na viongozi waandamizi wa UM na Kiongozi Mkuu wa Kuwait kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Kuwait

Mkutano wa pili wa kimataifa wa usaidizi wa kibinadamu kwa Syria umemalizika hukoKuwait ambapo zaidi ya dola Bilioni 2.4 zimechangishwa ikiwa ni ahadi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo amesema kiasi kamili cha fedha kitatangazwa baadaye lakini ahadi hiyo ni ishara dhahiri kuwa wahanga wa mzozo [...]

15/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na idadi ya vifo inayoongezeka Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kuendelea kuongezeka idadi ya watu wanaopoteza maisha nchini Sudan Kusini siyo jambo la kufumbiwa macho.   Amesema kuwa taarifa za watu kuendelea kupoteza maisha ikiwemo na wale 200 walioaga dunia baada ya mashuayaokuzama maji, ni taarifa zinazosikitisha na hivyo pande zinazozozana ziwajibike kuwalinda raia. [...]

15/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa MONUSCO alaani mashambulizi ya Mayi Mayi

Kusikiliza / Martin kobler

Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa MONUSCO amelaani vikali mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Mayi Mayi walioshambulia eneo la Pinga lililoko Kaskazini mwa jimbo la Kivu. Katika shambulizi hilo lililotokea hapo siku ya jumatatu askari wanne walipoteza maisha na raia watatu walijeruhiwa. Akielezea kusikitishwa kwake kutokana na hali hiyo, Martin Kobler amesema kuwa kuna [...]

15/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kundi la kwanza la walinda amani wa kuimarisha UNMISS lawasili Juba

Kusikiliza / Askari wa Nepal wakiwasili Juba tayari kuimarisha kikosi cha UNMISS

Kundi la kwanza la askari wa kulinda amani wanaopelekwa kuimarisha kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS limewasili kwenye mji mkuuJuba. Kundihilola askari 25 wa Nepal akiwemo afisa mmoja linatoka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH. Taarifa ya UNMISS inasema kundihiloni tangulizi na litafuatiwa na askari wengine [...]

15/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Matukio ya uharamia baharini yapungua

Kusikiliza / Uharamia

Kiwango cha vitendo vya uharamia baharini kimepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi duniani ndani ya miaka Sita na hiyo imeripotiwa kuchochewa na harakati za kudhibiti vitendo hivyo. Ofisi ya kimataifa dhidi ya uharamia na ile ya biashara zinasema mwaka jana pekee kulikuwa na matukio 264 duniani, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 40 tangu uharamia [...]

15/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongamano la kimataifa lamulika uzuiaji wa uhalifu wa mauaji ya kimbari

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York limefanyika kongamano la kimataifa kuhusu uelewa wa tahadhari za mapema kuhusu mauaji ya halaiki, ikiwa ni miaka ishiri imepita tangu kufanyika mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Joshua Mmali amefuatilia mazungumzo katika kongamano hilo TAARIFA YA JOSHUA Kongamano hilo lenye kauli mbiu: "mauaji ya kimbari [...]

15/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo Syria yana mkwamo, michango yahitajika hima: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Kiongozi Mkuu wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Ahmed Al-Jaber Al-Sabah kwenye mkutano wa kimataifa wa usaidizi kwa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amezungumza katika mkutano wa pili wa kuchangisha fedha kwa ajili ya misaada ya kiutu kwa watu wa Syria,  mkutano unaofanyika Kuwait ambapo Ban amesisitiza michango hiyo ni muhimu sasa kwa kuwa mzozo unaendelea na kusababaisha mkwamo wa kimaendeleo na uvunjifu wa haki za binadamu. Taarifa zaidi [...]

15/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Japan kuipa msaada Sudan Kusini wa dolla milioni 25

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema nchi yake inajiandaa kutoa msaada wa haraka wa dola takribani milioni 25 kwa Sudan Kusini kukabiliana na hali ya kibinadamu inayozidi kuzorota. Abe akizungumza wakati wa ziara yake nchini Ethiopia baada ya kutoka Ivory Coast na Msumbiji amesema dola milioni 20 kati ya milioni 25 wanazotoa zitatumika katika [...]

15/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay aomba ushirikiano wa kikanda ili kuwatia mbaroni wahalifu watoro

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ametoa wito kwa viongozi wanaokutana katika mkutano wa ukanda wa Maziwa Makuu, ICGLR, wahakikishe kuwa watu wanaoshukiwa kutekeleza uhalifu wa kimataifa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hawaendelei kukwepa mkono wa sheria kwa kuvuka mipaka na kukimbilia nchi jirani. Bi Pillay amesema [...]

15/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa nchi zinazoendelea wahitaji vichocheo ili uzidi kuimarika: Benki ya dunia

Kusikiliza / chati ya uchumi wa dunia

Miaka mitano baada ya mdororo wa uchumi, Benki ya dunia inasema kuwa kuna viashiria dhahiri kwa uchumi wa dunia kuanza kurejea hali ya kawaida huku nchi zinazoendelea nazo zikimulikwa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Ripoti ya hivi karibuni zaidi ya Benki hiyo kuhusu matarajio ya uchumi wa dunia inaweka bayana kuwa mwelekeo [...]

15/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bunge la Uganda laridhia uwepo wa UPDF Sudan Kusini

Kusikiliza / Bunge la Uganda katika kikao cha kujadili hoja ya kupelekwa kwa UPDF Sudan Kusini

Bunge laUganda limeridhia uwepo wa jeshi la serikali yaUgandakatika nchi jirani ya Sudan Kusini inaayokumbana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, ikiwa ni wiki kadhaa baada ya shutuma dhidi ya uamuzi wa RaisYoweri Museveni kupeleka majeshi bila ridhaa ya bunge. Hatua hiyo inakuja wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni likitoa taarifa [...]

15/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031