Nyumbani » 14/01/2014 Entries posted on “Januari 14th, 2014”

Kampeni kimataifa dhidi ya bidhaa bandia yazinduliwa: UNODC

Kusikiliza / NEMBO

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti w madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC imezindua kampeni mpya ya kimataifa ya kuibua uelewa juu ya madhara  ya usafirishaji haramu wa bidhaa bandia. Kampeni hii kupitia matangazo ya umma inaitwa, Bandia, usinunue na kutumbukia kwenye uhalifu wa kupangwa, na ina lengo la kuelimisha wanunuzi wa bidhaa [...]

14/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Waziri wa Iran wa masuala ya nchi za Kiarabu na Afrika

Kusikiliza / Hossein Amir Abdollahian na Ban Ki-moon wakati wa mkutano wao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Hossein Amir Abdollahian, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran anayehusika na masuala ya nchi za Kiarabu na Afrika. Katika mkutano huo ambao ulifanyika pembezoni mwa kongamano la pili la kutoa ahadi za ufadhili kwa ajili [...]

14/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ataka amani Misri ikipiga kura ya maoni

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anafuatilia kwa karibu mchakato wa kura ya maoni nchini Misri. Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Katibu mkuu mjini New York imemkariri Bwana Ban akisema anasisitiza umuhimu wa kuheshimu uhuru wa kukusanyika na kujieleza pamoja na ahadi ya kutofanya vurugu. Katibu mkuu amewhamasisha raia [...]

14/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Makamu Rais Benki ya dunia kanda ya Afrika kuzuru Angola

Kusikiliza / Makhtar Diop, Makamu Rais wa Benki ya dunia, Ukanda wa Afrika

Makamu Rais wa benki ya dunia kwa ukanda wa Afrika Makhtar Diop Jumatano anaanza ziara ya siku mbili nchiniAngola, lengo likiwa ni mazungumzo ya masuala ya maendeleo na Rais José Eduardo dosSantos, na viongozi wengine waandamizi wakiwemo mawaziri na Gavana wa Benki kuu. Taarifa ya Benki ya dunia imesema ziara yake, ya kwanza nchini humo [...]

14/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ECOSOC yapata Rais mpya, azungumzia malengo ya maendeleo ya milenia

Kusikiliza / Rais mpya wa ECOSOC, Balozi Martin Sajdik wa Austria

Baraza la kijamii na kiuchumi la Umoja wa Mataifa, ECOSOC leo limepata Rais mpya Martin Sajdik, ambaye ni mwakilishi wa kudumu waAustriakwenye Umoja wa Mataifa. Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Balozi Néstor Osorio, mwakilishi wa kudumu waColombiakwenye Umoja wa Mataifa ambaye amemaliza muda wake. Mara baada ya kuchaguliwa, Balozi Sajdik alizungumza na waandishi wa habari [...]

14/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Changamoto wanazokumbana nazo wahamiaji zaangaziwa

Kusikiliza / Wahamiaji eneo la Cara Mineo

Vijana, wake kwa waume hukimbia makwao kutokana na usalama au kusaka maisha bora na wakati mwingi hukumbana na changamoto nyingi wakati wakitafuta hifadhi katika nchi zingine haswa zilizostawi. Licha ya kwamba changamoto ni nyingi lakini kambi za muda wanayowekwa wahamiaji hawa kila uchao hupkea watu wapya je ni yapi wanayowakumba wahamiaji hawa basi ungana na [...]

14/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Afisa wa haki za binadamu kuzuru Sudan Kusini:

Kusikiliza / Ivan Šimonović,

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu Ivan Šimonović, anazuru Sudan Kusini kuanzia leo htarehe 14 Januari hadi tarehe 17 Januari ili kutathimini hali ya haki za binadamu nchini humo, athari za mapigano ya karibuni na kubaini maeneo ya kuboresha hasa pale ambapo raia wameathirika. Katika ziara yake ya siku nne Šimonović akiwa Juba [...]

14/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yaanza kurejesha nyumbani raia wa Mali kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / IOM inatoa kipaumbele kwa wale wenye mahitaji ya haraka hususan wagonjwa.

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM linaanza kusafirisha kwa ndege takribani wahamiaji 550 wa Mali waliokuwa wanaishi Jamhuri ya Afrika ya Kati na hiyo ni kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo na kutishia maishayao. Mpango huo unafuatia ombi la serikali yaMaliambapo ndege mbili zitaanzia safari Bangui hadi mji mkuu wa Mali,Bamako. Msafara huo unakuja baada [...]

14/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya milioni 3 wafaidika na msaada wa chakula wa WFP Syria:

Kusikiliza / WFP , Syria

Shirika la mpango wa chakula lduniani WFP limegawanya msaada wa chakula kwa watu miliioni 3.8 kwa mwezi wa Desemba na kuweka rekodi ya kipekee. Sasa shirika hilo linaendelea kuimarisha operesheni zake za kiufundi ili kulisha watu milioni Saba mwezi huu wa Januari.Idadi hiyo inajumuisha watu milioni 4.25 walio ndani yaSyriana zaidi ya milioni 2.9 waliopata [...]

14/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mary Robinson ahitimisha ziara yake DRC

Kusikiliza / Mary Robinson

Mjumbe maalum wa Umoja  wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu, Mary Robinson, amekamilisha ziara yake ya siku tatu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC. Hapo Jumatatu alikutana na Rais Joseph Kabila na waziri mkuu Augustin Matata Ponyo. Bi. Robinson alionesha furaha yake kwa mpango wa kupokonya silaha waasi na kujumuisha kwenye jamii, au [...]

14/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS na Global Fund wahofia sheria mpya Nigeria kuathiri vita dhidi ya ukimwi:

Kusikiliza / LGBT

Shirika la Umoja wa Mataifa la linalohusika na ukimwi UNAIDS na fuko la kimataifa la kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria Global Fund, wameelezea hofu yao dhidi ya fursa ya huduma kwa waathirika wa ukimwi ambao ni wasagaji, mashoga, wanaoshiriki mapenzi ya jinsia tofauti tofauti na waliobadili jinsia (LGBT), kwamba itaathirika pakubwa kutokana na [...]

14/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto kupata fursa kuwasilisha malalamiko yao mbele ya UM

Kusikiliza / Haki za watoto zinakiukwa wakati wanatumikishwa jeshini

Itifaki ya ziada kwa mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto imeridhiwa na nchi ya 10 na hivyo kuweka nuru zaidi kwa fursa ya watoto kuwasilisha malalamiko yao ya kunyanyaswa mbele ya kamati ya Umoja wa Mataifa. Itifaki hiyo ya ziada kwa mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto itaanza kutumika miezi mitatu ijayo ambapo [...]

14/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Raia zaidi wakimbia makwao Sudan Kusini:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini

Raia zaidi wa Sudan Kusini wanaendelea kuzihama nyumba zao na kuvuka mpka kuingia mataifa ya jirani ya Uganda, Ethiopia, Kenya na Sudan limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Shirika hilo linasema tangu katikati ya mwezi Decemba mwaka jana watu zaidi ya 78,000 wamekimbilia nchi jirani, na zaidi ya nusu ya watu [...]

14/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unatendeka CAR:UM

Kusikiliza / Rupert Coliville

Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu yakiwemo mauaji, ukatili wa kimapenzi,watu kukatwakatwa, kutoweka kunyanyaswa, ubakaji na mashambulizi ya kulenga raia makusudi kwa misingi ya kidini umekuwa ukitendeka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati , kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) [...]

14/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atembelea wakimbizi wa Syria nchini Iraq

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Mkuu wa UNHCR wakiwa kwenye moja ya mahema huko kambi ya Kawrgosik nchini Iraq.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameongoza ujumbe mzito kwenye kambi ya Kawrgosik,  eneo la Kurdistan nchini Iraq ambayo inahifadhi wakimbizi kutoka Syria, katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa shirika la wakimbizi duniani, UNHCR. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Bwana Ban ameshuhudia hali halisi kwenye kambi hiyo akisema amesikitishwa sana [...]

14/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031