Nyumbani » 13/01/2014 Entries posted on “Januari 13th, 2014”

Makazi mapya kwa wakimbizi yaandaliwa, mji wa Bor washikilwia na waasi: UNMISS

Kusikiliza / Martin Nesirky

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS unaandaa eneo jipya la makazi kwa wakimbizi wa ndani kutokana na kuendelea kumiminika kwa raia wa nchi hiyo kunakosababishwa na mapigano  yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini humo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa hivi sasa UNMISS [...]

13/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkakati wa amani, usalama na Ushirikiano bado ndio matumaini ya ukanda wa Maziwa Makuu: Bi Robinson

Kusikiliza / Wakati wa kikao cha Baraza la Usalama

Mwakilishi Maalum wa Katibu mkuu kuhusu ukanda wa Maziwa Makuu, Mary Robinson, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kuwa manthari ya matumaini yaloghubika hali mashariki mwa Kongo kufuatia kutia saini makubaliano yalotokana na mkutano ulioongozwa na rais Museveni wa Uganda na Rais Joyce Banda wa Malawi, sasa yametoweka, kwani ukanda wa Maziwa [...]

13/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Elimu inayotolewa kwa ufadhili wa UNICEF kambini nchini Afghanistan ni ya kutumainisha

Kusikiliza / Watoto wa Afghanistan

Elimu ni muhimu katika mustakhabali wa maisha ya kila mtoto na ni kwa sababu hii UNICEF inaendesha mafunzo katika familia ambazo zimejikuta katika kambi,  licha ya kuwepo amani bado watu hawa wanakabiliwa na changa moto nyingi katika masiha ya kila siku  basi ungana na Joseph Msami katika ripoti ifuatayo.  

13/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamhuri ya Afrika ya Kati iko katika kipindi muhimu: Babacar Gaye

Kusikiliza / Maisha yakiendelea kama kawaida mjini Bangui, baada ya kuanza kwa uongozi mpya wa mpito. (Picha  Serge Nya-Nana/BINUCA )

Jamhuri ya Afrika ya Kati iko katika kipindi muhimu hivi sasa kitakachoamua hatma ya nchi hiyo, amesema mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika  ya Kati, Jenerali Babacar Gaye alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, kwa njia ya simu kutoka mji mkuu Bangui. Amesema baada ya kujiuzulu [...]

13/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini inaweza kutumbukia kwenye tatizo la njaa-FAO

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya kuwa hali ya mapigano inayoendelea sasa huko Sudan Kusini inaweza inaweza kusababisha kuzuka kitisho cha njaa . FAO inasema kuwa hali ya misaada ya kibinadamu nchini humo kwa wakati huu imeendelea kuzorota na kwamba kunauwezekano mamia ya raia wakaendelea kupoteza maisha kutokana na kukosa mahitaji muhimu. Mapigano hayo [...]

13/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni muhimu kujitoa ili kulinda mafanikio ya kiusalama mashariki mwa DRC: Kobler

Kusikiliza / Martin Kobler, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa MONUSCO,

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo kujadili hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, huku Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO akionya kuwa ni vyema kuendeleza kasi ya mafanikio yalopatikana kiusalama ili eneo la mashariki lisitumbukie tena katika mikono ya waasi. Joshua Mmali na taarifa kamili TAARIFA YA [...]

13/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yapanua wigo wa usaidizi Sudan Kusini, yalalama kuporwa kwa vifaa

Kusikiliza / Wakati wa kupakua chakula kilichotolewa na WFP mji Mkuu wa Sudan Kusini, Juba

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limezindua operesheni mpya za usaidizi wa kibinadmau kwa waathirika wa mapigano huko Sudan Kusini, huku likishughulikia changamoto zinazokwamisha kufikia wale wanaohitaji misaada zaidi. Grace kaneiya na taarifa kamili   (TAARIFA YA GRACE KANEIYA)   Kiasi cha dola za Marekani milioni 57.8 kimetengwa ili kufanikisha operesheni hiyo itayodumu kwa [...]

13/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

India yasherehekea miaka mitatu bila Polio

Kusikiliza / Mtoto apewa chanjo

Nchini India leo ni miaka mitatu tangu kisa cha mwisho cha ugonjwa wa Polio kiripotiwe nchini humo na hivyo kuashiria mafanikio makubwa ya kuutokomeza ugonjwa huo hatari. George Njogopa na taarifa kamili (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)  Huku ikiendelea kutegemea ripoti za uchunguzi za kimaabara za mwezi Disemba na January, shirika la afya ulimwenguni WHO linajiandaa [...]

13/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kay aitaka Puntland kudumisha utulivu baada ya kubaduilishana madaraka:

Kusikiliza / Rais mteule Abdiweli Mohamed Ali Gaas

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, Jumapili ametoa wito wa kudumika amani na kufuata sheria baada ya kukabidhiana madaraka huko Puntland kufuatia uchaguzi wa Rais uliofanyika Januari 8. Bwana Kay amesema wabunge wa Puntland wamekuwa ni mfano wa kuigwa siku chache zilizopita kwa kuonyesha uwajibikaji, amani na uwazi katika uchaguzi. Pia [...]

13/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake wa Syria watoa mependekezo yao kuhusu mkutano ujao wa kimataifa

Kusikiliza / Wanawake wa Syria wakati wa maandamano Mei 2011(picha ya faili)

Mkutano wa siku mbili wa kuunga mkono ujumuishaji wa wanawake wa Syria katika harakati za amani Syria umemalizika mjiniGeneva, huku wanawake hao wakitoa mapendekezo muhimu kwa kile wanachotaka kuona wakati wa mkutano wa kimataifa ujao kuhusuSyria. Katika taarifa ilotolewa mwishoni mwa mkutano huo ambao uliandaliwa na kitengo kinachoshughulikia maswala ya wanawake, UN Women na serikali [...]

13/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mitandao ya kijamii yaweza kujenga au kubomoa haki za mtoto: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amefungua mkutano wa kamati ya mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC huko Geneva, Uswisi na kusema kuwa mitandao ya kijamii inaweza kujenga au kubomoa haki za mtoto iwapo haitaangaziwa vyema. Amesema kupitia mitandao hiyo, watoto na hata jamii wanaweza kupata taarifa [...]

13/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aitaka serikali ya Kenya kulinda haki za wanaofurushwa Msitu wa Embobut

Kusikiliza / James Anaya

Mtaalam huru wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Kenya kulinda haki za watu wa jamii ya kiasili ya Sengwer, ambao wanaripotiwa kukabiliwa na hatari ya kufurushwa kutoka kwenye msitu wa Embobut kwenye milima ya Cherangani magharibi mwa Kenya. Mtaalamu huyo kuhusu haki za watu wa asili, James Anaya amesema amesikitishwa [...]

13/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asema hali ya Iraq inamtia hofu, asema jukumu ni la wanasiasa

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Kamel Al-Malik

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Kamel Al-Malik mjini Bagdhad,Iraq hii leo ambapo wameangazia masuala kadhaa ikiwemoSyria, hali nchiniIraqna uhusiano kati ya nchi hiyo naKuwait. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.  (Taarifa ya Assumpta) Wakati wa mazungumzo hayo Bwana Ban amerejelea tena hofu yake kuhusu [...]

13/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu kufanya kikao maalumu kuhusu CAR

Kusikiliza / Baraza la haki za binadamu

  Baraza la haki za binadamu litafanya kikao maalumu Jumatatu tarehe 20 Januari kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ombi la kufanyika kikao hicho limewasilishwa leo kwa njia ya barua na mwakilishi wa Ethiopia kwenye baraza hilo kwa niaba ya kundi la Afrika. Barua hiyo imetiwa saini nchi wanachama [...]

13/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF na WHO walaani uingiliaji wa chanjo ya polio Al-Raga Syria

Kusikiliza / Mtoto apokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio

 Wawakilishi wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO, wamelaani vikali kitendo ya kuingilia kampeni ya chanjo ya polio kwenye jimbo la Al-Raqa nchini Syria kutokana na mapigano makali miongoni mwa makundi yenye silaha. WHO na UNICEF wanasaidia kuhakikisha kwamba kila mtoto nchiniSyriaanapata chanjo bila kujali ni [...]

13/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031