Nyumbani » 10/01/2014 Entries posted on “Januari 10th, 2014”

Baraza la usalama lashutumu yanayoendelea Iraq

Kusikiliza / Zaid Ra'ad Zedi Al Hassan

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo wamekuwa na kikao kuhusu hali ilivyo nchiniIraqambapo wameshutumu ghasia za hivi karibuni kwenye maeneo ya Fallujah na Ramadi kwenye jimbo la Anbar nchini Iraq. Katika kikao kilichofanyika jioni ya leo, Rais wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Januari balozi Zaid Ra'ad Zedi Al Hassan [...]

10/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasema mzozo wa Sudan Kusini usiingiliwe na majeshi ya kigeni

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakinyoosha mkono kupiga kura

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likisema mzozo wa Sudan Kusini hautakiwi kuingiliwa na nguvu za kijeshi za kigeni. Taarifa hiyo inafuatia mkutano wa Baraza hilo hapo jana, ambapo lilisikiliza ripoti za Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani, Hervé Ladsous, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa ujumbe [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kupambana na ukimwi zamulikwa nchini Burundi na Tanzania

Kusikiliza / UNAIDS

Mnamo Alhamisi wiki hii, Kongamano la ngazi ya juu limefanyika huko Washington DC likiangazia vichocheo vya kijamii vinavyoweza kusaidia kutokomeza Ukimwi na umaskini uliokithiri. Katika kongamanohiloambalo lilijumuisha Benki ya Dunia, Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP na Shirika linalokabiliana na Ukimwi, UNAIDS, Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Michel Sidibé alisema kuwa  mabilioni ya dola yanayoelekezwa kwenye [...]

10/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wasaidia mafunzo ya polisi magereza nchini Somalia

UNSOM

Mafunzo ya siku tatu kwa ajili ya polisi nchiniSomalia  yanaendelea mjiniMogadishuchini ya usaidizi wa ofisi ya umoja wa mataifa nchini humo UNSOM na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC. Washiriki ni polisi wanaohusika na uangalizi wa wafungwa magerezani na wale wanaoshikiliwa rumande. Taarifa ya UNSOM inasema kuwa [...]

10/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF na wadau wajizatiti kuwakinga watoto dhidi ya magonwja huko Chad

Kusikiliza / Mtoto apewa chanjo

Mizozo inayoendelea kwenye maeneo mbali mbali barani Afrika imesababisha wakimbizi kuhama na hivyo kubadili ratiba ya maisha yao ikiwemo kupatiwa chanjo. Huko Chad, wakimbizi kutoka Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati wamejikuta kwenye maeneo tete na kukosa huduma muhimu kama vile chanjo kwa watoto. Je ni wapi huko na nini kinafanyika kuhakikisha watoto wanapata haki [...]

10/01/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Syria ni muhimu zaidi sasa: OCHA

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kiutu OCHA imesema mkutano wa pili wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kuinusuru Syria utakaofanyika mjini Kuwait wiki ijayo ni muhimu hasa kwa kuzingatia kuwa hali ya kiutu nchini humo ni tete na inazidi kuzorota. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva leo msemaji wa [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR inasaka taarifa zaidi za ripoti za boti zilizo na wahamiaji kutoruhisiwa kuingia Australia

Kusikiliza / Nembo ya UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatafuta taarifa zaidi kutoka uongozi wa Australia kuhusu ripoti za karibuni kwenye vyombo vya habari kwamba jeshi la maji wa Australia linazilazimisha boti zinazoshukiwa kubeba waomba hifadhi zinazotaka kuingia nchini humo kurejeaIndonesia. Pia linafuatilia habari kwamba Australia ina mipango ya kununua na kutoa meli zitakazotumika siku [...]

10/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kamati ya IPU yakutana kushughulikia masuala ya haki za binadamu za wabunge

Kusikiliza / Nembo ya IPU

Kesi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu za wabunge 262 zitatathminiwa na Kamati ya Haki za Binadamu ya Muungano wa Wabunge Duniani, IPU, wakati itakapokutana wiki ijayo mjini Geneva. Kamati hiyo ambayo itakutana kuanzia tarehe 13-17 Januari, pia itachunguza uwezekano wa kuwepo kesi nyingine zinazohusisha mauaji ya wabunge, kukamatwa kiholela na kubinywa kwa uhuru wa [...]

10/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Senegal yakaribia kutokomeza mbun'go

Kusikiliza / Madume tasa ya mbung'o huachiwa hewani mara ili kupunguza uzao wa wadudu hao

Mradi unaotekelezwa na shirika la kilimo na chakula duniani, FAO nchiniSenegalwenye lengo la kutokomeza mbung'o umeanza kuonyesha dalili ya kushinda vita dhidi ya wadudu hao hatari kwa mifugo. Meneja mradi huo kutoka Wizara ya Mifugo Baba Sall amesema tangu kuanza kwa mradi mwaka 2012, idadi ya wadudu hao imepungua kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la [...]

10/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vitendo vya uporaji na ukiukwaji mwingine lazima ukome Sudan Kusini:UM

Kusikiliza / UNMISS

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zote kuwezesha operesheni za mpango wa Umoja wa mataifa Sudan Kusini  UNMISS na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu . Ombi hilo linajumuisha kuheshimu majengo na vituo vya Umoja wa mataifa, vifaa namalizao, kuheshimu shughuli za misaada ya kibinadamu , wafanyakazi namaliwakati wote. Umoja wa Mataifa umeongeza kuwa [...]

10/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa amani na maridhiano watoa wito wa amani Sudan Kusini

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini wakiwa kambini

Viongozi wa makundi ya kikabila wa taasisi za amani na maridhiano kwa pamoja Alhamisi kwa mara ya kwanza wamewataka viongozi wa kisiasa Sudan Kusini kusitisha mapigano mara moja na kuweka mpango wa mani. Nguzo tatu za kitaifa zinazojumuisha serikali, bunge, jumuiya za kijamii na viongozi wa wanaowakilisha jamii mbalimbali wamewataka wanasiasa kujihusisha katika mchakato wa [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM kuanza kuwasafirisha wahamiaji walioko CAR.

Kusikiliza / Wananchi waliosaka hifadhi kwenye uwanja wa ndege kwenye mji mkuu Bangui, CAR (Picha-IOM)

Shirika la uhamiaji duniani IOM, kesho linatarajia kuanza kuwasafirisha kwa ndege maelfu ya wahamiaji wa nchi mbalimbali walioko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambao wametatizika kufuatia mgogoro unaoendelea nchini humo. Zaidi ya wahamiaji Elfu 60 kutoka nchi jirani wameshapelekea maombi kwenye balozi zao CAR. IOM imepokea maombi ya kuwaondoa wahamiaji kutoka Chad , [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2014 uwe wa juhudi zaidi dhidi ya migogoro, umaskini na mabadiliko ya tabianchi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema mwaka huu mpya unahitaji juhudi zaidi kidiplomasia, hatua zaidi dhidi ya umaskini na pia kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Bwana Ban amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York, ambako amezungumzia masuala muhimu yatakayoangaziwa mwaka. Bwana Ban amesema mwaka huu pia [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuharamisha COMANGO Malaysia kunatia wasiwasi:UM

Kusikiliza / rights

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema inatiwa wasiwasi na uamuzi wa karibuni wa wizara ya mambo ya ndani ya Malaysia kutangaza kwamba muungano wa jumuiya 54 za kijamii ujulikanao kama COMANGO nchini humo ni haramu. Taarifa ya Grace Kaneiya Inabainisha zaidi (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Tarehe nane Januari mwaka huu wizara [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mali ina fursa ya kujikwamua kiuchumi baada ya mzozo: IMF

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji Christine Lagarde akiwa Bamako, Mali

Shirika la Fedha duniani, IMF limesema Mali baada ya mapigano inaweza kuibuka na kujikwamua kiuchumi iwapo tu itaweza kutambua na kufungua fursa ilizonazo. Taarifa zaidi na Joseph Msami. (Taarifa ya Msami) Kidole kimoja hakiokoti  jiwe, methali maarufu nchiniMali ambayo Mkurugtenzi Mtendaji wa IMF Christine Lagarde aliitumia kuhitimisha hotuba yake mbele ya wajumbe wa baraza la [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasaka dola milioni 99 kwa ajili ya Sudan Kusini na CAR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Bangui walokimbilia uwanja wa ndege, CAR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa ombi la dola milioni 99 ili kuwasaidia maelfu ya watu waliotawanywa na machafuko na hali mbaya Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR. Fedha hizo ni kwa ajili ya watu wa Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati waliofungasha virago na kuzikimbia [...]

10/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yazidi kutiwa hofu na usalama wa wakimbizi wa ndani Sudan Kusini

Kusikiliza / UNHCR ikiwasaidia wakimbizi wa Sudan Kusini

Zaidi ya watu 231,000  wametawanywa na machafuko hadi sasa Sudan Kusini tangu yalipozuka Desemba 15 mwaka jana imesema ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Kwa mujibu wa ofisi hiyo watu wengine 43,000 wamekimbilia mataifa jirani yaKenya,Uganda,SudannaEthiopia. OCHA inasema takribani watu 60,500 [...]

10/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031