Nyumbani » 09/01/2014 Entries posted on “Januari 9th, 2014”

Mwelekeo wa kuimarisha kikosi cha UNMISS ni mzuri: Ladsous

Kusikiliza / Hervé Ladsous akizungumza na waandishi wa habari

Mwelekeo wa kutekeleza azimio la Baraza la Usalama kuhusu kuimarisha kikosi chake cha ulinzi wa amani Sudan Kusini, UNMISS uko sawa licha ya shaka zinazodaiwa kuwa zilijitokeza. Amesema Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mashauriano ya faragha ya baraza [...]

09/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka mataifa kuchangia fedha za kuinusuru Syria

Kusikiliza / wakimbizi wa syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi wanachama wa umoja huo kuhudhuria katika kongamano la pili la kutoa ahadi za ufadhili kwa ajili ya misaada ya kiutu kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu na kuimarisha Syria na nchi jirani zake, ikiwemo Lebanon. Akiongea mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu Farhan Haq [...]

09/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Plumbly akutana na Waziri wa Kuwait kabla ya kongamano la wafadhili

Kusikiliza / Derek Plumbly

Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Derek Plumbly, amekutana leo na Waziri Mtendaji wa Masuala ya Kijamii wa Kuwait, Wael Abou Faour kujadili maandalizi ya kongamano la wafadhili nchini humo, ambalo limepangwa kufanyika mnamo tarehe 15 Januari. Kongamano hilo la kutoa ahadi za ufadhili limeandaliwa na Mfalme wa Kuwait, Sheikh Sabah Al Ahmed [...]

09/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awataka viongozi wa nchi za kati mwa Afrika kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameyaambia mataifa ya ukanda wa kati mwa Afrika kuwa anasikitishwa sana na kuenea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo hilo, na kutaka mzunguko wa machafuko na ulipizaji kisasi miongoni mwa jamii vikomeshwe mara moja. Bwana Ban amesema hayo katika ujumbe wake kwa mkutano wa jumuiya [...]

09/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Familia zilizopoteza makazi Syria zaonana na mkuu wa WFP

Kusikiliza / Mkuu wa WFP Bi. Ertharin Cousin akizungumza na mtoto mkimbizi wa ndani huko Damascus, Syria

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin amehitimisha ziara yake ya siku moja nchini Syria iliyomkutanisha na viongozi wa ngazi za juu serikalini na familia zilizopo mji mkuu Damascus baada ya kupoteza makazi  yao kutokana na mapigano. Familia hizo ni zile zinazopata mgao wa chakula mjini humo ambapo Bi. Cousin [...]

09/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Onesho la ubunifu wa mitindo ya mavazi lafanyika UM

Kusikiliza / Wabunifu wa mitindo waliongia fainali

Ukifikiria Umoja wa Mataifa hapana shaka unawaza juu ya jamii mbalimbali, tamaduni zao na tofuti zao zikiwa pamoja katika taasisi hii ya kimataifa. Na pia hapana shaka unawaza kuhusu masuala ya kisiasa na diplomasia ya kimataifa. Sio rahisi kuwaza kuhusu maonesho ya ubunifu wa mitindo ya mavazi katika Umoja huo. Kulikoni? Ungana na Joseph Msami [...]

09/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mkakati wa kutokomeza njaa wazinduliwa nchini Timor-Leste

Kusikiliza / Nembo

Mkakati wa kwanza wa kutokomeza njaa katika ukanda wa Asia na Pasifiki umezinduliwa leo nchini Timor-Leste na Waziri Mkuu wa taifa hilo, Kay Rala Xanana Gusmão. Mkakati huo ambao kwanza ulizinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon mnamo mwaka 2012, unalenga kuweka mustakhbali ambao watu wote wanafurahia haki ya kuwa na chakula, [...]

09/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNMISS atembelea Malakal kujionea hali halisi

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson akizungumza na wakimbizi walioko kituo cha UNMISS huko Malakal

Takribani mwezi mmoja tangu kuanza kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson amefanya ziara ya kwanza kwenye mji mkuu wa jimbo la Upper Nile, Malakal, ili kujionea hali halisi. Akiwa ziarani humo alitembelea eneo ambalo ujumbe wa Umoja wa [...]

09/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IPU yakaribisha makubaliano ya kisiasa kuhusu ulinzi wa wabunge wa Uturuki

Kusikiliza / IPU jengo

Muungano wa Kimatatifa wa Wabunge, IPU, umekaribisha makubaliano yalofikiwa wiki hii na vyama vitatu vya kisiasa nchini Uturuki ya kufanyia marekebisho katiba ya kitaifa ili iweke wazi ni katika mazingira yepi afisa aliyechaguliwa anaweza kushtakiwa au kufungwa. Makubaliano hayo yanatazamia kupanua uwanja wa ulinzi wa wabunge na kutatua tatizo la wabunge kadhaa waliofungwa, kwa mujibu [...]

09/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vichocheo vya kijamii ni muhimu kujumuishwa ili kuondokana na Ukimwi na Umaskini

Kusikiliza / Moja ya kampeni za kukabiliana na Ukimwi.

Kongamano la ngazi ya juu linafanyika huko Washington DC, nchini Marekani likiangazia vichocheo vya kijamii vinavyoweza kusaidia kutokomeza Ukimwi na umaskini uliokithiri. Ripoti ya Joshua Mmali  inafafanua zaidi. (Ripoti ya Joshua) Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo Benki ya Dunia, shirika la mpango wa maendeleo-UNDP na lile linalokabiliana na Ukimwi, UNAIDS walitoa mada [...]

09/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uganda yatathmini ardhi inayozozaniwa na wananchi na wakimbizi

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC walioko Uganda

Nchini Uganda kazi imeanza ya kufungua mpaka wa ardhi inayozozaniwa kati ya wakimbizi wanaoishi kambi ya Kyangwali na wananchi wa eneo hilo. Miongoni mwa wakimbizi hao ni wale wanaotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kama anavyoripoti John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, Uganda. (Tarifa ya John Kibego) Ufurushwaji wa zaidi ya watu [...]

09/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei ya chakula duniani ingali ya juu japo haijayumba:FAO

Kusikiliza / Soko la Chakula

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema bei ya chakula duniani bado ni ya juu na mwaka 2013 ni miongoni ya miaka iliyoweka rekodi ya gharama ya juu ya chakula. Flora Nducha na maelezo zaidi. (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Kwa mujibu wa orodha ya gharama za chakula ya FAO mwezi Desemba mwaka 2013 wastani ulikuwa [...]

09/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Visa vingine 7 vya mafua ya A H7N9 vyabainika kwa binadamu China:WHO

Kusikiliza / Utafiti maabarani

Tume ya kitaifa ya afya na mpango wa familia Uchina imelifahamisha shirika la afya duniani WHO kuthibitishwa kwa visa vingine saba vya maambukizi ya virusi vya mafua ya ndege, A(H7N9) kwa binadamu. Tarehe 4 Januari taarifa ya kuugua kwa ajuza wa miaka 86 mjini Shangai zililipotiwa kwa WHO. Alianza kuumwa Desemba 26 na kulazwa hospital [...]

09/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa ndani Sudan Kusini waweka makao kwenye kituo UNMISS

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini

Karibu mwezi mmoja tangu kuzuka kwa mapigano Sudan Kusini maelfu ya raia wamechukua hifadhi katika makambi ya mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo UNMISS mjini Juba na hawana dalili ya kurejea makwao. Baadhi ya wakimbizi hao wa ndani wanaosema wanajihisi salama zaidi wakiishi kwenye maskani ya UNMISS kuliko majumbani kwao, wameanzisha biashara ya kuuza [...]

09/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031