Nyumbani » 08/01/2014 Entries posted on “Januari 8th, 2014”

Maelfu ya wakimbizi toka Sudani Kusini wazidi kumiminika Uganda

Kusikiliza / wakimbizi.2jpg

Wakati machafuko nchini Sudani Kusini yakiendelea wakimbizi wanaoikimbia nchini humo wanaendelea kumiminika sehemu mbalimbali ikiwamo nchi jirani kama Uganda ambapo maelfu wanaripotiwa kukimbilia nchini humo.  John Kibego wa radio washirika Spice Fm ya nchini Ugandaamesafiri hadi katika kambi iitwayo Kiriandongo kujionea hali ilivyo na kuandaa ripoti ifuatayo.  

08/01/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Bi. Kaag apatia Baraza la Usalama ripoti kuhusu Syria

Kusikiliza / Sigrid Kaag

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo wakati wa mashauriano ya faragha, wamepatiwa taarifa kuhusu maendeleo ya uteketezaji wa mpango wa silaha za kemikali nchini Syria ikiwa ni siku moja baada ya ripoti ya kwamba shehena ya kwanza yenye vifaa vinavyohusiana na mpango huo imeondolewa nchini humo. Taarifa hizo zimetolewa na Sigrid [...]

08/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wahaha kuwanusuru wakimbizi nchini Iraq.

Kusikiliza / Nembo ya Umoja wa Mataifa

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov amesema umoja huo unafanya kazi kwa karibu na mamlaka za kitaifa na kikanda nchini Iraq pamoja na washirika wa misaada ya kiutu kuhakikisha misaada ya kiutu na ya dharura inawafikia salama watu waliokwama pamoja na familia zilizopoteza makazi katika jimbo liitwalo Anbar. [...]

08/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bolivia yachukua uenyekiti wa G-77

Kusikiliza / Katibu Mkuu akutana na rais wa Bolivia Evo Morales Ayma

Leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imefanyika hafla ya kukabidhi uongozi kwa mwenyekiti mpya wa Muungano wa  G 77 na Uchina, wenye nchi wanachama 133.  Wadhfa huo ambao umekuwa ukishikiliwa na taifa la Fiji, sasa umekabidhiwa Bolivia. Kwa maelezo zaidi, hii hapa taarifa ya Joshua Mmali. (TAARIFA YA JOSHUA) Katika hafla hiyo ya [...]

08/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaanza tena kuwasambazia misaada watu waliohamia uwanja wa ndege Bangui

Kusikiliza / Wakimbizi wa CAR waliokimbia makwao

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeanza tena hapo jana kusambaza misaada ya kibinadamu kwa watu wapatao 100,000 walolazimika kuhama makwao, na ambao sasa wamepiga kambi kwenye uwanja wa ndege mjini Bangui, katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Shughuli ya ugawaji misaada ya kibinadamu ililazimika kuahirishwa mara kadhaa kwa sababu za kiusalama, [...]

08/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yahakikisha majeruhi Sudan Kusini wanapata tiba sahihi

Kusikiliza / Wagonjwa wakipatiwa huduma katika hospitali ya Juba huko Sudan Kusini

Mapigano yanayoendelea nchiniSudan Kusini yamesababisha majeruhi zaidi ya 2,500 ambapo shirika la afya duniani, WHO na wadau wake linahakikisha wanapata matibabu sahihi pamoja na usaidizi wa vifaa tiba vinavyotakiwa. WHO inasema inahakikisha majeruhi wanaohitaji tiba zaidi wanahamishiwa hospitali zenye uwezo ikiwemo ile yaJubaambako kuna madaktari bingwa wa upasuaji na hata wa tiba za kisaikolojia. Miongoni mwao [...]

08/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misaada ya haraka yahitajika CAR kunusuru wakimbizi :UM

Kusikiliza / Wakimbizi wa CAR wapokea msaada kutoka UNHCR

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa kutoa kwa haraka raslimali toshelevu kwa ajili ya kulinda na kusaidia mahitaji ya idadi kubwa na inayokuwa ya watu waliopoteza makazi kufuatia ghasia katika jamahuri ya Afrika ya Kati, CAR. Amesema mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za watu waliopoteza makazi Chaloka Beyani. Katika taarifa yake Bwana [...]

08/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi Sudan Kusini watoa ushirikiano kulinda mustakhbali wao: UNHCR

Kusikiliza / Mfanyakazi wa UNHCR azungumza na wanawake kuhusu kugawa bidhaa za kujisafi katika jimbo la Upper Nile

Wakimbizi wa ndani huko Sudan Kusini wamejikuta wakilazimika kusaidiana na wafanyakazi wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR ili kuziba pengo la watendaji na kuhakikisha majukumu ya kuwapatia usaidizi yanafanyika bila kikwazo chochote. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Ripoti ya Assumpta) Mkuu wa operesheni za shirika hilo kwenye eneo la Bunj jimbo la [...]

08/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO imeaanza kugawa mbegu kwa wakulima walioathirika na kimbunga Haiyan Ufilipino

Kusikiliza / Waziri wa maswala ya kigeni wa Norway Børge Brende, akiwa na wakulima Ufilipino

Miezi miwili baada ya kimbunga Haiyan kukumba Ufilipino waziri wa mambo ya nje wa Norway Børge Brende, amelipongeza shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO kwa kazi yake ya kuwasaidia wakulima wa mpunga kwa mbegu ili kuziba pengo la mazo waliyopoteza kwenye kimbunga. Brende amewatembelea wakulima wa kijiji cha Tingib jimbo la [...]

08/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Somalia aipongeza Puntland

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay amempongeza Rais mteule wa Puntland. Abdiweli Mohamed Ali Gaas, aliyeteuliwa leo Jumatano na wajumbe wa wabunge wa Puntland. Grace Kaneiya na taarifa kamili (TAARIFA YA GRACE) Bwana Kay amesema anampongeza spika na wabunge wote kwa juhudi zao za kuelekea mchakato wa amani wa kura ya [...]

08/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaanza tena kuwalisha wakimbizi wa ndani CAR

Kusikiliza / WFP yawasilisha mgao wa chakula CAR

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeanza tena kugawa chakula kwa familia za wakimbizi wa ndani kwenye uwanja wa ndege wa Bangui nchini Jamhuri ya Afrijka ya kati ambako inasemekana watu wapatao 100,000 wamepata hifadhi. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Ugawaji huo umeanza tena baada ya [...]

08/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031