Nyumbani » 06/01/2014 Entries posted on “Januari 6th, 2014”

Takriban nusu ya watu wote CAR wanahitaji msaada wa kibinadamu: Feltman

Kusikiliza / Jeffrey Feltman

Hali katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imezorota kwa kiasi kikubwa huku takriban watu milioni 2.2 wakihitaji misaada ya kibinadamu, amesema Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman, wakati akilihutubia Baraza la Usalama. Bwana Feltman amesema idadi hiyo ni karibu nusu ya idadi nzima ya watu nchini humo, huku nusu ya watu [...]

06/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yatoa usaidizi kwa wapiganaji waliojisalimisha DRC

Kusikiliza / Wakati wa zoezi la kutoa msaada, DRC

Zoezi la usaidizi kwa wapiganaji wanaojisalimisha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC linaendelea ambapo wapiganaji hao wanajumuishwa katika jamii huku wengine wakijumuishwa katika jeshi la serikali kwa hiari. Joseph Msami anamulika zoezi hili huko mashariki mwa DRC katika makala inayoangazia namna ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC unavyosaidia kuweka utulivu katika nchi hiyo iliyokumbwa [...]

06/01/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na vifo nchini Bangladesh, atoa wito kwa vyama vya siasa

Kusikiliza / Ramana ya Bangladesh

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza kusikitishwa kwake na vifo vilivyotokea nchini Bangladesh pamoja na matukio ya vurugu wakati wa uchaguzi wa wabunge siku ya jumapili, uchaguzi ambao amesema ulighubikwa na mvutano na ushiriki wa wapiga kura ulikuwa ni mdogo. Ameeleza masikitiko yake kuwa vyama husika vilishindwa kuafikiana juu ya mambo ambayo [...]

06/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban atuma mialiko kwa washiriki kwenye kongamano kuhusu Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametuma nyaraka za mialiko kwa WaSyria na washiriki wa kimataifa kwenye kongamano kuhusu Syria, ambalo linatarajiwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi kuanzia Januari 22, 2014. Orodha ya washiriki kwenye kongamanohiloiliamuliwa mnamo tarehe 20 Disemba kwenye mkutano ulohusisha Marekani, Urusi na Umoja wa Mataifa. Kongamano hilo limetokana na [...]

06/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama huko Bor, Juba Sudan Kusini bado ni tete

Kusikiliza / Farhan Haq

Hali bado si shwari kwenye eneo la Bor, jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, ni kauli ya Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York. Amesema kusini mwa mji huo mapigano makali yameripotiwa kati ya majeshi ya serikali na yale ya upinzani ambapo makazi ya ujumbe wa Umoja [...]

06/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

China yateketeza tani 6.2 za meno ya tembo

Kusikiliza / Uteketezaji wa tembo China

Biashara ya magendo ya meno ya tembo imekuwa na madhara makubwa kwa tembo wa Afrika, amesema Mtendaji Mkuu wa Mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa biashara ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka CITES, John Scalon huko Guangzhou, China hii leo wakati wa shughuli za kuteketeza tani Sita nukta Mbili za meno ya viumbe hao.   Bwana [...]

06/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yaendelea kuwaondoa wahamiaji wa Chad walioko CAR

Kusikiliza / Wahamiaji katika uwanja wa ndege wa Bangui wanaokimbia mapigano CAR IOM inawasaiidia kuhama

Leo tarehe sita Januari imekuwa siku ya 16 tangu Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM lilipoanza kuwasafirisha wahamiaji wa Chad kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, huku wahamiaji 493 wakichukuliwa kwa ndege mbili kutoka mji mkuu wa CAR, Bangui. Idadi ya wahamiaji wa Chad walionusuriwa kutoka CAR tangu tarehe 21 Disemba sasa imefikia watu [...]

06/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo kuhusu Sudan Kusini bado yakumbwa na mkwamo

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini

Idadi ya watu wanaokimbia Sudan Kusini kukwepa mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya serikali na wafuasi wa makamu wa rais wa zamani imeongezeka na kufikia Laki Moja na Elfu Themanini na Tisa huku baadhi yao wakisaka hifadhi nchi jirani. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya raia Elfu Ishirini [...]

06/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Michezo yaweza kukuza ajira kwa vijana: ILO

Kusikiliza / Watoto wakicheza kandanda

Shirika la kazi duniani, ILO, linasema waajiri walio wengi hukwepa kuwaajri vijana wengi  kwa  kigezo cha ukosefu wa  ujuzi wa kazi huku wengi wakiwa hawazingatii kwamba vijana wanaweza kupata ajira iwapo waajiri watazingatia ujuzi wao katika michezo. Kwa mujibu wa mtaalamu wa ajira za vijana wa ILO kanda ya Asia na Pacific Matthieu Cognac ujuzi [...]

06/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay akaribisha uamuzi wa mahakama kuu Nepal

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay amekaribisha uamuzi wa mahakama kuu ya Nepa luliotolewa tarehe mbili mwezi huu ukitaka msamaha usitolewe kwa makosa ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliotekelezwa katika miaka 10 ya vita nchini humo. Grace Kaneiya na taarifa kamili.  (TAARIFA YA GRACE KANEIYA)  Bi Pillay [...]

06/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waziri mkuu wa Somalia akutana na mwakilishi wa UM

Kusikiliza / Nicholas Kay

Waziri mkuu mpya wa Somalia amekutana kwa mara ya kwanza na mwakilishi wa Umoja wa mataifa nchini humo Nicholas Kay mwishoni mwa wiki tangu aliposhika wadhifa huo. Waziri Abdiweli Sheikh Ahmed amemshukuru Bwana Kay kwa Umoja wa mataifa kuendelea kusaidia ujenzi mpya wa Somalia na anatarajia kuendelea kuwepo kwa ushirikiano mzuri katika siku za usoni. [...]

06/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031