Nyumbani » 02/01/2014 Entries posted on “Januari 2nd, 2014”

Ban, Baraza la usalama walaani shambulio huko Mogadishu

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na wajumbe wa Baraza la Usalama wamelaani vikali shambulio la Jumatanombele ya mgahawa wa Jazeera  huko Mogadishu nchini Somalia uliosababisha vifo na majeruhi. Katika taarifa zao zilizotolewa kwa nyakati tofauti, Bwana Ban na wajumbe hao wametuma risala za rambirambi kwa wafia wa shambulio hilo huku wakiwatakia ahueni [...]

02/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani yaanza kurejea Mali, wakimbizi waanza kurejea

Kusikiliza / Wakimbizi wakijiandikisha

Kuimarika kwa amani nchini Mali hivi karibuni kumesababisha baadhi ya wakimbizi wa nchi hiyo walioko Niger kuanza kurudi makwao. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na mashirika mengine linaratibu mchakato huo. Joseph Msamia anaangazia zoezi la kuondoka kwa wakimbizi hao katika makala ifutayo. Ungana naye.  

02/01/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani shambulizi la bomu Beirut

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama wakinyoosha mkono kupiga kura

  Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la bomu lililotekelezwa leo Januari 2 kusini wa Beirut nchini Lebanon, na ambalo liliwaua watu wapatao 5 na kuwajeruhi wengine wengi.  Wanachama hao wa Baraza la Usalama wametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wahanga na kutoa pole zao kwa wote [...]

02/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usaidizi wa dharura umeongezeka na kuuweka UM kwenye majaribio: OCHA

Kusikiliza / Mkuu wa masuala ya usaidizi wa kibinadamu ndani ya UM Bi. Valerie Amos

Idadi kubwa ya watu ambayo haijawahi kutokea wanaanza mwaka mpya wakiwa ni wakimbizi wa ndani au wamekimbilia nchi jirani na hivyo kuwa ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Mataifa kwenye utoaji usaidizi wa kibinadamu. Hiyo ni kauli ya Mkuu wa masuala ya usaidizi wa kibinadamu ndani ya umoja wa Mataifa Valerie Amos aliyotoa mjiniNew York, [...]

02/01/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu alaani shambulio la Beirut, Lebanon

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani vikali shambulio la leo kwenye kitongoji cha Haret Hreik, kusini mwa mji mkuu wa Lebanon,Beirut. Bwana Ban amekaririwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa akieleza kuwa mlipuko huo wa  bomu kwenye gari uliosababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi umetokea siku chache baada ya shambulio lingine [...]

02/01/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WHO na wadau wazindua kampeni dhidi ya Surua, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Surua

Baada ya taasisi moja nchini Jamhuri ya Afrika  ya Kati, CAR kuthibitisha uwepo wa wagonjwa wa surua kwenye kambi mbili za wakimbizi wa ndani nchini humo, mashirika ya umoja wa Mataifa na wadau wamezindua kampeni ya dharura ya kudhibiti ugonjwa huo. Mashirika hayo ni pamoja na lile la afya, WHO, watoto UNICEF na lile la [...]

02/01/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Fao yawasaidia wakulima wa Ufilipino kujikwamua baada ya Kimbunga Haiyan

Kusikiliza / Kimbunga Haiyan kilikwamisha juhudi za kilimo

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, limeanza kuwapa afueni wakulima wapatao 44,000 nchini Ufilipino, ambao waliathiriwa na kimbunga Haiyan, kwa kuwapa mbegu zenye ubora wa hali ya juu ili kuwasaidia kujikwamua tena baada ya uharibifu wa kimbunga hicho mnamo Novemba 8, 2013. Taifa la Ufilipino lilipoathiriwa na kimbunga Haiyan, wakulima walikuwa wanajiandaa kwa mavuno ya [...]

02/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kutokomeza ukeketaji zinaenda kwa mwendo wa pole: WHO

Kusikiliza / Ukeketaji bado haukatokomezwa: WHO

Hatua za kutokomeza ukeketaji wa wanawake zimekuwa zikiendelea kwa mwendo wa pole sana, na juhudi zaidi zinahitajika katika ngazi za kisiasa na kijamii ili kutokomeza desturi hiyo. Hayo yamechapishwa kwenye jarida la Shirika la Afya Duniani, WHO, ambalo limesema wanawake wapatao milioni 125 walio hai wamepitia ukeketaji wa aina moja au nyingine. Wengi wa wanawake [...]

02/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vifo vitokanavyo na ugaidi vyaongezeka Iraq, UM waonya

Kusikiliza / UNAMA

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMA, umetoa takwimu zinazoonyesha kuongezeka kwa mauaji yatokanayo na ugaidi kwa mwaka 2013 ambapo kwa mwezi December pekee watu 759 waliuwawa huku 1345 wakijeruhiwa. Katika orodha hiyo ya vifo UNAMA inasema  raia ni 661 wakiwemo polisi jamii 175 huku pia katika idadi ya wale waliojeruhiwa raia ni 1201 [...]

02/01/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yatoa wito kwa jamii za Sudan Kusini kudumisha utengamano

Kusikiliza / Jamii ya waSudan Kusini

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, ametoa wito wa kwa jamii za Sudan Kusini kuheshimu minyambuliko ya kijamii, huku akielezea masikitiko makubwa kufuatia kuongezeka kwa machafuko nchini humo. Assumpta Massoi na taarifa kamili (TAARIFA YA ASSUMPTA) Bi Bokova amelaani kuuawa kwa watu na kuongezeka uhasama miongoni mwa jamii tofauti, [...]

02/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mapigano Sudan Kusini bado yanaendelea: UNMISS

Kusikiliza / Raia wa Sudan Kusini wakiwa kwenye kambi ya muda nchini mwao baada ya kukimbia makazi yao

Habari kutoka Sudan Kusini zinasema kuwa mapigano bado yanaendelea hususan jimbo la Unity na Jonglei. Afisa kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS Joseph Contreras ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa mapigano hayo ni kwenye mji wa Mayone jimbo la Unity na kwenye viunga vya mji wa Bor huko [...]

02/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya mtoto wa kwanza kuzaliwa mwaka mpya huko Tacloban si nzuri

Kusikiliza / Mtoto aliyezaliwa akiwa na mama yake aitwaye  Vivian Aplaca. (UNFPA)

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu, UNFPA limesema hali ya kiafya ya mtoto wa kwanza kuzaliwa mwaka mpya 2014 huko Tacloban, nchini Ufilipino si nzuri pamoja na mama yake. Shirika hilo linasema mama huyo Vivian Aplaca alijifungua salama kwa upasuaji kwenye kituo cha Visayas ambacho kilipatiwa vifaa vya kisasa na UNFPA [...]

02/01/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini iko njiapanda, hatma yake iko mikononi mwa wanasiasa: UNMISS

Kusikiliza / Hilde Johnson, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Sudan Kusini

Sudan Kusini iko njiapanda lakini bado kuna fursa ya kuepusha mwendelezo wa ghasia na mapigano, amesema Hilde Johnson mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo na pia mkuu wa ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani  UNMISS. Taarifa zaidi na Joshua Mmali. (Taarifa ya Joshua) Katika salamu zake za mwaka mpya [...]

02/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasudan Kusini 7600 waingia Uganda kufuatia mapigano nchini mwao

Kusikiliza / Raia wa Sudan Kusini waliokimbia makwao kutokana na mapigano

Mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini yamesababisha raia kuendelea kukimbia nchi hiyo na ripoti za hivi karibuni zinakariri kuwa zaidi ya raia 7600 wamekimbilia nchiniUgandawakati huu ambapo Umoja wa Mataifa na nchi za Afrika zinaendelea na jitihada za kupata suluhu la kisiasa kwenye mzozo huo. Kwa tarifa kamili, tungane na John Kibego wa redio washirika ya [...]

02/01/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031