WFP yasambaza mafuta kwa Wasyria kunapoanza msimu wa baridi

Kusikiliza /

Mtoto wa Syria

Huku watu nchini Syria wakikabiliana na msimu wa baridi kali shirika la mpango wa  chakula duniani WFP limeanza shughuli  za usambazaji wa karibu tani 10,000 za mafuta kwa wakimbizi wa ndani wanaoishi kwenye maeneo kumi ya mji wa Damascus.

Mafuta yanayosambaza nayo  yatatumika kwenye upishi  na kwa kupasha joto. Usambazaji zaidi wa mafuta unapangwa kufanywa kwenye sehemu 35 za mji wa Homs, Hama na vitongoji vya mji wa Damascus siku  zinazokuja.

WFP imesambaza migao 3000 ya chakula kinachoweza kulisha watu 15,000 kwa kipindi cha mwezi mmoja ikiwa pia na mpango wa kutoa chakula kwa watu milioni 4  mwezi huu kote nchini Syria.

Makundi ya kutoa misaada hayajafanikiwa kufika eneo la Al Hassakeh kwa muda wa miezi mitano iliyopita kutokana na kuwepo ukosefu wa usalama barabarani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930