Watu wapatao 100 yasemekana kuuawa huko DRC; MONUSCO yachunguza

Kusikiliza /

Mkuu wa MONUSCO Martin Kobler

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO umeripoti kuwa watu wapatao Mia Moja yasemekana waliuawa wakati wa mashambulio ya jana kwenye mji mkuu  Kinshasa, Lubumbashi na Kindu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amemkariri Mkuu wa MONUSCO na mwakilishi wa Katibu Mkuu huko DR Congo, Martin Kobler akisema kuwa wanaendelea kuchunguza ripoti hizo. Kwa mujibu wa Martin, Kobler ameshutumu vikali mashambulio hayo yaliyofanywa na watu wenye silaha na ametaka serikali kuchukua hatua haraka dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo kwa mujibu wa katiba na sheria. MONUSCO imerejea kauli yake kuwa mashambulizi dhidi ya raia yanapaswa kukoma na kuitaka serikali itoea taarifa kuhusu mashambulio hayo huku MONUSCO ikiimarisha ulinzi kwenye maeneo yake na yale ya raia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031